Skip to main content

Posts

Showing posts from June 23, 2024

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo n...

UWANDANI CHAKE CHAKE WAKUMBUSHWA KUTOZITIA MKONO KESI ZA JINAI

    NA MWANDISHI WETU, PEMBA@@@@ WANANCHI wa shehia ya Uwandani wilaya ya Chake chake Pemba, wamekumbushwa kujitenga mbali na sulhu za kesi za jiani, ikiwemo za udhalilishaji, kwani kufanya hivyo, ni kuyapalilia matukio hayo. Hayo yameelezwa leo Juni 25, 2024 na Mkuu wa Divisheni ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar ofisi ya Pemba, Bakar Ali Omar, kwenye hutuba iliyosomwa kwa niaba yake na Msaidizi wa sheria wa Jimbo la Wawi Haji Nassor, kwenye mkutano wa wazi, kwa wananchi waliomo ndani ya mpango wa kanusuru kaya maskini, ikiwa ni sehemu ya wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar. Alisema, bado wapo baadhi ya wazazi, wamekuwa wakizikalia mkekani kesi hizo, kwa kuzifanyia sulhu, jambo ambalo kisheria ni kosa na kuongeza kichocheo kwa watendaji. ‘’Niwasihi sana wananchi wa Uwandani, tukiwa ndani ya wiki ya msaada wa kisheria, jambo hilo mliepuke na ikitokezea mkimbile mbele ya vyombo vya sheria,’’alieleza. Katika hatua nyingine, aliwataka wananchi hao, kuwatumia wasai...

UHALIFU MFIKIWA CHAKE CHAKE BADO KITENDAWILI

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa shehia ya Mfikiwa wilaya ya Chake chake, wamesema kupooza kwa ulinzi shirikishi katika shehia yao, kumesababisha kurudi upya vitendo vya kihalifu, ikiwemo wizi wa mifugo. Walisema, kwa sasa wapo wafugaji wanaolazimika kulala na mifugo yao majumbani kama vile Ng’ombe kutokana na kuhofia wizi ulioshamiri shehiani hapo. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kijijini hapo, Juni 22, 2024  walisema, kwa sasa hali ya vitendo vya kihalifu imeibuka upya, kufuatia ulinzi shirikishi kutoonekana. Walieleza kuwa, kwa sasa ndani ya shehia yao hakuna ndizi, muhogo, fenesi, chungwa wala mifugo ya kuku, Ng’ombe na Mbuzi wanaonawiri kwa wizi ulivyokithiri. Mmoja kati ya wananchi hao Mohamed Khamis Ali, alieleza kuwa, kwa miaka zaidi ya sita sasa, hakuna tena ulinzi shirikishi ambao uliondoa vitendo vya uhalifu. ‘’Sasa hakuna mkulima wala mfugaji anaefaidika na mazao yake, kutokana na wizi uliokithiri ambao ni watu kutoka ndani ya shehia yet...

WAMBAA, CHUMBAGENI KUANZISHA MFUKO WA UCHINJAJI

    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WAUMINI wa dini ya kiislamu shehi za Wambaa na Chumbageni wilaya ya Mkoani Pemba, wamekutana na kukubaliana kuanzisha mfuko maalum wa uchinjaji, kila ifikapo mfunguo tatu, kwa ajili ya sadaka kwa wasiokua na uwezo. Kwenye kikao hicho, kilichofanyika skuli ya Wambaa, waumini hao walisema, imeonekana kuna kundi kubwa kubwa la waumini wenzao, wamekuwa kikosa kitoweleo kwa siku za sikukuu, jambo ambalo sio sahihi. Akizungumza Mwenyekiti wa muda wa mfuko huo Ali Abdi Mohamed, jana Juni 22, 2024  alisema wamekusudia kuwa mfuko huo uwasaidie, wale ambao uwezo wao uko chini. Alieleza kuwa, mpango huo wa uchinjaji kila ifikapo mfunguo tatu, kwa hatua za awali utahusisha kila watu saba, kutakiwa kumiliki Ng’ombe mmoja na kumuwasilisha kwa kamati, kwa ajili ya uchinjaji. Mwenyekiti huyo alisema, kisha baada ya kukamilisha taratibu za uchinjaji, kutagawiwa mafungu matatu, kama sheria ya dini ya kiislamu ilivyoelekeza, ambapo fungu moja hutolewa...