Skip to main content

Posts

Showing posts from June 18, 2023

MCT KUTAANGAZA WATEULE WA EJAT 2022 WIKI HII

  Majina ya wateule wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2022, yanatarajiwa kujulikana Juni 23, 2023 katika kikao kati ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) na waandishi wa habari kitakachofanyika katika ukumbi wa hotel ya The Diplomat ya jijini Arusha. Katika mashindano hayo, jumla ya kazi 893 ziliwasilishwa kutoka vyombo vya habari vya magazeti, radio, runinga na vyombo vya habari vya mtandaoni. Jopo la majaji saba, wenye utaalamu katika habari radio, runinga, magazeti na vyombo vya habari vya mtandaoni walifanya kazi kwa siku tisa ili kupitia kazi hizo. Majaji hao wakiwa chini ya Mwenyekiti, Mkumbwa Ally walifanya kazi hiyo kuanzia Juni 10 mara baada ya kuapishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Baraza la  Habari Tanzania (MCT) Jaji mstaafu wa Mahakama Kuu, Robert Makaramba  Juni 9, 2023. Jopo hilo lilikuwa na wajumbe wafuatao Rose Haji Mwalimu, Mbaraka Islam, Peter Nyanje, Nasima Chum, Dk. Egbert Mkoko na Mwanzo Millinga aliyekuwa Katibu wa jopo hilo. Washindi

WAANDISHI WA HABARI 272, VYOMBO VYA HABARI 94 VYAKUMBWA NA MADHILA TANZANIA

  Ikiwa ni miaka 30 tangu Mei 3 ya kila mwaka ilipotangazwa kuwa siku rasmi ya kuadhimisha Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani (WPFD) na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA) mwaka 1993, matukio mengi ya madhila dhidi ya uhuru wa waandishi na vyombo vya habari hapa nchini yameendelea kutotolewa taarifa. Waandishi wa habari wamechukulia kukumbana na madhila kama unyanyaswaji, kupigwa, kunyang’anywa vifaa, na kutishiwa kama ‘ajali kazini’ na hivyo kutoyatolea taarifa. Msukumo wa taarifa umekuwa ukiwekwa kwenye matukio makubwa yanayohusisha kujeruhiwa, kutekwa ama kupoteza maisha; hivyo taarifa nyingi za madhila hazipo kwenye kumbukumbu.   Uanzishwaji wa Kanzidata na Malengo yake Kutokana na changamoto hii, mwanzoni mwa mwaka 2012 Baraza la Habari Tanzania (MCT) lilianzisha kanzidata ya kitaifa kwa ajili ya kurekodi  madhila wanayopata waandishi wa habari ama vyombo vya habari. Lengo likiwa ni kuwa na ushahidi wa kitakwimu na uhalisia kwa ajili ya kufanya uchechemuzi  wenye ushahidi. Mal