BY MUNIRA KAONEKA, ZANZIBAR@@@@ Katika jitihada za kuimarisha uhifadhi wa mikoko na matumizi endelevu ya rasilimali za asili, Jumuiya ya Community Forests Pemba (CFP) imefungua mafunzo maalum kwa Watoa Mafunzo ya Jamii (ToTs) kuhusu uhifadhi wa mikoko na usimamizi wa rasilimali za jamii. Mafunzo haya, yalifanyika kuanzia tarehe 19 hadi 21 Februari katika ofisi za CFP Unguja, na yalilenga kuwawezesha washiriki kuwa viongozi wa uhifadhi wa mazingira katika jamii zao. Mafunzo haya yameandaliwa ili kuongeza uelewa wa washiriki kuhusu umuhimu wa mikoko, mbinu za kuhifadhi misitu, na namna ya kushiriki katika usimamizi wa rasilimali za asili kwa njia endelevu. Kupitia mafunzo haya, ToTs watapata ujuzi wa vitendo na mbinu za kufundisha ambazo zitawawezesha kuwa mabalozi wa mabadiliko katika maeneo yao. Akifungua rasmi mafunzo haya, Mkurugenzi Mtendaji wa CFP alisisitiza kuwa uhifadhi wa mikoko ni jukumu la jamii nzima. “Uhifadhi wa mikoko na urejeshwaji wake ni kazi ya pamoja, na ni...