NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI 112, wakiwemo wanawake 80 na wanaume 32 wa shehia ya Uwandani wilaya ya Chake chake, wamejitokeza na kupewa elimu, ushauri na msaada wa kisheria, uliotolewa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ katika kambi ya siku tatu. Akizungumza na blog ya pemba today juzi, Afisa Miradi wa ‘ZLSC’ Beny Louis Mlingi, alisema wengi wao ni wale waliolalamikia ukosefu wa vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya ndoa, vitambulisho vya ukaazi pamoja na migogoro ya ardhi. Alieleza kuwa, kwa sasa wamepanga kulifuatilia hilo, ili kuona wanawasaidia wananchi hao, ili kupata nyaraka hizo muhimu kwa ajili ya shughuli nyingine. ‘’Ni kweli hapa Uwandani wananchi wameitikia wito wa kufika kwenye kambi yetu ya siku tatu, na tumegundua shida zipo za wananchi kulalamikia ukosefu wa nyaraka muhimu,’’alifafanua. Mapema Mwenyekiti wa Kituo hicho Pfrofesa: Chriss Maina Peter, alisema wanakusudia kukutana na watendaji wakuu wa serikali, ili kuona wananchi hoa wasiokuwa na uwez...