Skip to main content

Posts

Showing posts from January 8, 2023

Internews-Trained Journalists shine in EJAT Awards 2022

By Alakok Mayombo and Temi Mahondo, Internews Tanzania:::::   FIVE journalists mentored by Internews’ Boresha Habari project have scooped seven of this year’s Excellence in Journalism Awards Tanzania (EJAT), held on May 28, 2022 in Dar es Salaam. Zanzibar print reporter and blogger Haji Mohamed won two first places and says Internews deserves a lot of credit for his success: “ I feel as if I should give one of my awards to Internews!   Their trainers offer so much more than theory. They follow up and mentor your field work, which really helps you to grow, as a journalist.”   Haji’s story on people with disabilities fighting for their rights through the courts won in the Disability category, while his ground-breaking report on the negative impact of traditional marriage dowries won in the Open category. Haji works for Zanzibar Leo newspaper, blogs at Pemba Today, and says the training he gets from the Boresha Habari program has given him new skills and boosted his confidence.  Radio rep

FAMILIA ZENYE WATOTO WENYE ULEMAVU PEMBA WAKUMBUSHWA JAMBO

    NA HAJI NASSOR, PEMBA:: WAZAZI na walezi kisiwani Pemba, wamekumbushwa kuwa, sio haki watoto wenye ulemavu kukoseshwa haki zao za msingi, kama elimu na kuchanganyika na wenzao, kwa sababu ya ulemavu walionao. Hayo yameelezwa na Mratibu wa Idara ya watu wenye ulemavu kisiwani humo, Mashavu Juma Mabrouk, wakati akizungumza na wazazi, walezi na wanafunzi wa madrssa za Umi ya Vikunguni na ile ya Annajah ya Machomane Chake chake, kwenye ziara iliyoandaliwa na Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar. Alisema, bado baadhi ya wazazi na walezi, wamekuwa wakijenga dhana kuwa, mtoto mwenye ulemavu anahiari ya kumpatia elimu, na asiyekuwa na ulemavu ndio mwenye haki kamili. Alieleza kuwa, dhana hiyo isiwapitikie wazazi hata siku moja katika maisha yao, na badala yake wawe na haki sawa watoto wenye ulemavu na wengine, ili kutimiza matakwa ya kisheria. Mratibu huyo alisema, suala la uwep wa changamoto kwenye sekta ya elimu kama vile uhaba wa vifaa visaidizi kwa watoto wenye ulem

IPA: 'WATUMISHI WA UMMA TUMIENI LUGHA MWANANA KWA WANANCHI'

  NA HAJI NASSOR, PEMBA::: WATUMISHI wa umma kisiwani Pemba, wametakiwa kutumia lugha laini, zenye mvuto, shirikishi na zenye heshima wakati wanapowahudumia wananchi wanaofika kwenye tasisi hizo kudai huduma. Hayo yameelezwa na Mkuu wa Chuo cha Utawala wa Umma ‘IPA’ tawi la Pemba Juma Haji Juma, wakati akizungumza na watumishi wa baraza la mji Chake chake, wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na wa wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, kwenye mafunzo ya sehemu ya uthibitisho wa kazini, yaliofanyika ukumbi wa Baraza la mji Chake chake. Alisema, moja ya msingi mkuu kwa watumishi wa umma, wakati wanapowahudumia wananchi, ni matumizi ya lugha sahihi na zenye ushawishi wa kupokea na kutoa huduma. Alisema, wapokea huduma huwa wanahitaji kusikilizwa, kushauriwa, kufafanuliwa na wakati mwengine kuelezwa jambo lilipofikia, ambapo mchakato wote huo, matumizi ya lugha nzuri ni jambo la kuzingatia. ‘’Niwakumbushe watumishi wenzangu wa umma kuwa, suala la kutumia lugha isiy

WANANCHI PEMBA WADAI KULAZIMISHWA CHANJO YA CORONA, WIZARA YATOA TAMKO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA::: WIZARA ya Afya Zanzibar, imepiga marufuku kwa daktari yeyote, kumlazimisha mwananchi kuchoma chanjo ya kinga ya Corona, na badala yake, chanjo hiyo itaendelea kuwa ya hiari ya mtu binafsi. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu Januari 13, 2023, Waziri wa wizara hiyo Zanzibar, Nassor Ahmed Mazurui, alisema hakuna mtu yeyote, mwenye mamlaka ya kumlazimisha mwengine, kuchanja chanjo hiyo. Alisema, bado kila mtu yuko huru ama kuamua kuchanja au kukataa kufanya hivyo, kwani suala la kinga ni la hiari ya mtu binafsi, na sio kumlazimisha kama ilivyozuka kwa baadhi ya madaktari kulalamikiwa. Alisema bado msimamo wa wizara ya Afya, ni kuona chanjo hiyo inakuwa ya hiari, na wala hukuna daktari yeyote wala mfanyakazi wa wizara, mwenye nguvu na mamlaka ya kumlazimisha mtu kuchanja. ‘’Kama kuna daktari anawalazimisha watu kuchanja chanjo ya Corona, hilo ni kosa kisheria, maana bado msimamo wa serikali kuwa chanjo hiyo, ni hiari,’’alisema. Ha

MAHAKIMU, WAENDESHA MASHTAKA: 'MSITULAUMU KESI ZINAPOFUTWA'

  NA HAJI NASSOR, PEMBA:: MAHAKIMU, waendesha mashtaka katika mahakama maalum ya kupmabana na ukatili na udhalilishaji kisiwani Pemba, wameiomba jamii kuacha kuwalaumu, pale kesi za aina hiyo, zinapofutwa au mtuhumiwa kuachiwa huru. Walisema, wao yapofanyika matendo hayo huwa hawapo eneo la tukio, hivyo hawajui kinachoendelea, na ndio maana wanategemeo wao kuwaeleza, lakini kama hawafiki mahakamani kutoa ushahidi, na kesi kufutwa, wasiangushiwe lawama. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kuelekea mwaka mpya wa mahakama 2023, walisema jamii ndio ambayo inategemewa mno, na mahakimu na waendesha mashataka, katika kufikia haki ya kweli. Walieleza kuwa, wao wapo kuwasubiri wananchi kufika mahakamani kuto ushahidi, hivyo kama wanakataa wito wa mahakama, kitakachofuata ni mtuhumiwa kuachiwa huru. Hakimu wa mahakama maalum ya kupambana na udhalilishaji mkoa wa kusini Pemba, Muumini Ali Juma, alisema kama jamii inajua namna wao wanavyokabiliana na wakati mgumu, ni kuwaonea huruma

SOKO LA ASALI LAJA ZANZIBAR

  WAZIRI  wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi   Rahma Kassim Ali amesema kuwepo kwa kituo cha usarifu wa asali   nchini kutaimarisha upatikanaji wa bidhaa hiyo na kuondokana kwa tatizo la                     kukosekana kwa soko la zao hilo hapa Zanzibar. Akizungumza katika uzinduzi wa kituo cha kusarifu asali huko Kizimbani Unguja Wilaya ya Magharibi "A"ikiwa ni shamrashamra za kuelekea miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Alisema ujenzi wa kituo hicho utawasaidia wajasiriamali wadogo wadogo kukuza kipato   pamoja na ajira kwa   makundi mbali mbali wakiwemo   vijana na wanawake.   Alisema kua ujenzi wa vituo hivyo ni muhimu kwa upande wa Unguja na Pemba ambapo ni miongoni mwa jitihada za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) katika kuimarisha rasmi Sekta ya Uwekezaji   kiuchumi ili kuleta tija kwa wananchi kwa ujumla. "Vituo hivyo vitasaidia sana kuwawezesha wananchi hasa wanawake kujikwamua kiuchumi na kuondokana kua tegemezi kwani watakua wamejiajiri na kuon

AMINA JUMA: MJASIRIAMALI ALIYEANZIA MBALI ,SASA AANZA KUONA BANDARI, UFUGAJI, KILIMO CHAMTOA

  NA HANIFA SALIM, PEMBA:: “HALI ya maisha yangu ilikua ni ngumu mno, na wakati mwengine ili kutimiza mahitaji, ilimlazimu muume wangu kuuza kuni,’’. Ni maneno ya mama mmoja mwenye familia ya watoto watano Amina Juma Salum (40) mkaazi wa kijiji cha Kwawema kilichopo shehia ya Mgogoni wilaya ya Micheweni Pemba. KABLA YA KUJIAJIRI Hali ya maisha yake ilikua ngumu kabla ya kuingia katika uanzishaji wa mradi mbali mbali, na hapo ndio mume wake ilimlazimika kutafuta kuni auze, ili kupata chakula walau kwa siku moja. Shida hata kwa watoto wake kupata elimu, walipokua wanakwenda skuli sare zao zilikua ni chafu, zimechanika na hata michango ya skuli ilikua inawashinda. “Ninapotokezewa na misiba au harusi nilikua najisikia vibaya mno, kwani nilishindwa kushirikiana na wenzangu katika michango ya kifedha, hadi pale ninaposuka makuti na kuuza ndipo huchangi”, anakumbuka.   Maisha hayo yalikua ni ya takribani miaka 17 na ndipo ulipoanza mradi wa kunusuru kaya maskini ambapo alipa