NA ZUHURA JUMA, PEMBA JAJI Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Abdalla amewataka mahakimu kuendelea na kasi ya kusikiliza kesi za udhalilishaji kwa haraka, ili ziweze kupata hatia kwa muda mfupi. Akiwasilisha ripoti ya ziara ya Jaji huyo iliyofanyika kuanzia Julai 18 mwaka huuu, Kaimu Mrajis Mahakama Kuu Zanzibar Salum Hassan Bakar alisema, takwimu zinaonesha kupungua kwa kiasi kikubwa mrundikano wa mashauri hayo mahakamani. Alisema kuwa, katika ripoti hiyo Jaji Mkuu aleleza kuwa, pamoja na kuridhika kwa kasi ya uendeshaji wa mashauri hayo kwa mahakama za udhalilishji Mkoa wa Kaskazini na Kusini Pemba, lakini bado mahakimu wana jukumu la kuziendesha kesi hizo kwa haraka zaidi. ‘’Vile vile aliridhishwa na ujaji wa mashahidi mahakamani na kuwaasa wale wachache ambao wanakaidi, wajitokeze kufika mahakamani ili kuyamaliza kabisa mashauri hayo’’, alisema Kaimu huyo. Aidha aliwaagiza mahakimu na makadhi kuyafanyia kazi mashauri yaliyofikishwa mahakamani kuanzia mwaka 2020 kuja c...