NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@@ MKUU wa mkoa wa kaskazini Pemba, Salama Mbarouk Khatib amesema vikao kazi kwa masheha na watendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ‘ZSSF’ vinasaidia kuongeza ushirikiano na ufanisi wa kazi. Alisema, unapokuwa karibu na ofisi ya tawala za Mikoa ndio umeifikia jamii kwa urahisi, na kiyume chake ni kudhoofisha utendaji kazi ofisi isiyotaka ushirikiano na masheha. Hayo yameelezwa leo Machi 7, 2025 na Mkuu wa wilaya ya Wete Abdalla Rashid Ali, kupitia hutuba ya Mkuu huyo mkoa, wakati wa ufunguzi wa kikao kazi, cha masheha na watendaji wa ZSSF, kilichofanyika ukumbi wa mikutano Jamhuri Wete. Alisema, ushirikiano huo ambao ‘ZSSF’ wameuomba ni eneo zuri la utendaji kazi, kwani chanzo cha jamii na kuifikia kwa haraka na wepesi ni uwepo wa masheha. Alieleza kuwa, kilichofanywa na ‘ZSSF’ kinaashiria umoja na mshikamo katika kufanikisha majukumu ya kila siku, yanayosimamiwa na viongozi wakuu wa nchi. Alifahamisha kuwa, ndani ya wilaya na mkoa, wamekuwa...