Skip to main content

Posts

Showing posts from July 10, 2022

WADAU PEMBA WATAJA MWARUBAINI WA AMANI ZANZIBAR

  NA HAJI NASSOR, PEMBA WADAU wa ujenzi wa amani kisiwani Pemba, wamesema kama haki itatendeka katika sekta kadhaa zilizopo Zanzibar, suala la uvunjifu wa amani, litabaki kwenye vitabu vya kumbu kumbu pekee. Walisema, bado kuna tasisi ndani ya serikali zimekuwa zikisababisha uvujifu wa amani, kwa kule kutotenda haki ipasavyo, wakati wanapowahudumia wananchi. Wakizungumza kwenye kongamano la amani na mashirikiano lililoandaliwa na tasisi ya Search for Common Ground ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa ‘dumisha amani Zanzibar’ na kufanyika ukumbi Greef Foullege Chake chake Pemba, walisema msingi wa amani ni haki. Walieleza kuwa, kazi inayofanywa na ‘ SCG’ kwa kushirikiana na ‘ the foundation for Civil Society’ kwa ufadhili wa Umoja wa nchi za Ulaya ‘EU’ ni nzuri, ingawa sasa kazi iliyobakia kwa watendaji ni kutekeleza haki. Mmoja kati ya wadau hao, kutoka Jumuiya ya Maimamu Zanzibar ‘JUMAZA’ Yussuf Ramadhan Abdalla, alisema uvunjifu wa amani hujitokeza baada ya m...

MTUHUMIWA KESI YA ULAWITI PEMBA AKATAA KUSOMEA KOSA LAKE

    NA FATMA HAMAD, PEMBA MAHAKAMA ya mkoa Chake Chake, imeghairisha   kesi ya   kuingilia kinyume na maumbile, inayomkabili kijana Khamis   Abdalla Khamis ‘kirare’ mwenye miaka [20], mkaazi   wa   Kangani   wilaya ya Mkoani, baada ya mtuhumiwa huyo   kukataa kusomewa shitaka lake.     Mtuhumiwa huyo wakati akiwa ametulia kizimbani hapo akisubiri kusomewe shitaka lake aliiambia mahakama hiyo kuwa, hali yake sio mzuri, anaomba   kesi ighairishwe na ipangiwe siku nyengine. ‘’Mheshimiwa hakimu leo, (jana) ninaumwa na siwezi kukakaa, hivyo naiomba mahakama yako ighairishe shauri langu, kwa leo na kulipangia siku nyingine,’’ alidai. Hakimu wa mahakama hiyo Muumin Ali Juma, alimueleza mtuhumiwa huyo kuwa,   hiyo ni haki yako   na inahitajika kupewa.   ‘’Lakini tu nikueleze leo shahidi ambae ni daktari amekuja wewe unasema unaumwa, ila   na siku akidharurika yeye   usijekulalamika, hivyo kwa leo tu...

WATAALAMU 'ECD' PEMBA WATAJA NJIA 5 KUKUZA UBONGO WA MTOTO

    NA HAJI NASSOR, PEMBA WATAALAMU wa malezi ya kisayansi, makuzi na uchangamshi wa mtoto katika hatua za awali ‘ECD’ kisiwani Pemba, wametaja njia tano ambazo familia ikizifuata, itakuwa ni chachu ya ukuaji wa ubongo kwa matoto na kuongeza ufahamu. Moja ya njia hizo ni chakula bora ikiwa ni pamoja na mboga mboga, matunda na samaki kwa mama mjamzito, tokea siku ya kwanza baada ya kubeba ujazito. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, walisema kwa mfano katika samaki, kuna kirutubisho kinachoitwa ‘omega three’ ambacho chenyewe kimebaba chembe chembe zinazoitwa ‘rids’ ambazo kazi yake kubwa, ni kujenga ubongo wa mtoto. Mmoja kati ya wataalamu hao Dk. Omar Adam Mohamed anayesomea matibabu ya watoto nchini China, alisema hatua nyingine, ni mama mjamzito kunywa maji kwa wingi. Alisema chumvi chumvi na kalshiam zilizomo ndani ya maji safi na salama, humsadiai mtoto kukukua kwa haraka na kujenga ubongo wake tokea akiwa tumboni. Mtaalamu huyo alisema, mama mjamzito...

KAMA TAMTHILIA VILE KESI YA DAKTARI IS-HAKA PEMBA KUACHIWA HURU

  NA HAJI NASSOR, PEMBA::: MTOTO wa miaka 16, ambae awali aliliambia Jeshi la Polisi kuwa, amebakwa na daktari Is-haka Rashid Hadid, na kisha kumkana mahakamani na kuondolewa kwa kesi hiyo, sasa mtoto huyo, anashikiliwa na Jeshi hilo, kwa kutoa taarifa za uongo. KESI HII ILIANZIA WAPI? Itakumbukwa kuwa, mtoto huyo miezi mitatu iliyopita, ndie aliyeliambia Jeshi la Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, kuwa ni daktari huyo pekee, ndie aliyemtorosha na kisha kumbaka zaidi ya mara moja. Baada ya maelezo ya mtoto huyo, ndipo Jeshi la Polisi lilipojitayarisha kirasilimali na kumfuata daktari huyo kijijini kwao Kangagani wilaya ya Wete, na kumkamata na kuanza kumuhoji. Baada ya kuhojiwa juu ya tuhma zinazomkabili, kisha daktari huyo, kuanzia Mei 18, mwaka huu alipandishwa Mahakamani na kuswekwa rumande, hadi Mahakama ya mkoa Wete ilipomuondoshea shataka dhidi yake juzi Julai 13, mwaka 2022. Ambapo Hakimu wa mahakama maalum ya makosa ya udhalilishaji mkoani humo, Ali Abdur-haman Ali...

NOELA: MTAALAMU WA KUZIDARZI NYWELE, SALUNI YAKE YAMPA UHAKIKA WA MAISHA

  NA MARYAM SALUM, PEMBA   “SHIDA, dhiki na maneno makali niliyoyapata wakati naishi kwa mjomba wangu, ndio chanzo cha kuamua kujiajiri,’’ndio maneno ya kwanza ya mjasiriamali Noela Alfred Majia mmiliki wa saluni ya Crassiana hair salun liyopo Gereji Wawi- Chake chake. Hapa ndio msemo ‘mtegemea cha ndugu hufa maskini’ ulipotafsirika kwa vitendo kwa mjasiriamali huyo mzaliwa wa Dar-es Salaam na sasa mkaazi wa Wawi Chake chake Pemba. HISTORIA YAKE Alikuwa anaishi na mama yake mzazi na mjomba wake, akimtegemea kwa kila kitu kwa wakati huo, huku mama yake akiwa na uwezo mdogo wa kuendesha familia. Noela alijihisi mtoto wa maana sana mbele ya mjomba wake, na aliamini anaweza kuwa mwanga wa maisha yake, hasa kwa vile ni mjomba anayetokana na mama yake mzazi. ‘’Kwa hakika tamaa ya kukaa na mjomba na kisha kuwa na maisha mazuri hapo baadae, nilifikiria sana, na sikutarajia kuwa iko siku mjomba engegeuka adui wa maisha yangu,’’anasema. Wakati Noela akiwa na miaka 17 alis...

ALIYEDAI KUBAKWA NA DAKTARI PEMBA SASA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI

  HABARI zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa, daktari Is-haka Rashid Hadid ameachiwa huru na Mahakama ya Mkoa Wete. Sababu kubwa ya kuachiwa ni pale mtoto aliyedai kubakwa na daktari huyo, kumkana mahakamani wakati akitoa ushahidi wake. Makubwa zaidi sasa Jeshi la Polisi linamshikilia mtoto huyo kwa kulidanganya Jeshi la Polisi Je...unahitaji habari hii kwa upana wake endelea kufuatilia www.pembatoday.blogspot.com

UTPC: WAANDISHI WA HABARI ZINGATIENI USALAMA WENU MNAPOKUWA KAZINI

  NA ZUHURA JUMA, DODOMA WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kuzingatia usalama wao wakati wanapofanya kazi ya kuandika habari, kwani ni maisha yao ni muhimu zaidi kuliko habari hizo. Akifungua mafunzo ya siku mbili juu ya ulinzi na usalama kwa waandishi huko Dodoma, Mjumbe wa Bodi ya UTPC Yussuf Mussa alisema, mafunzo hayo yatawajengea uwezo waandishi katika kujitambua na kujua thamani yao katika utendaji wa kazi zao za kihabari. Alisema kuwa, waandishi wa habari wamekuwa na jukumu kubwa la kuwapasha wananchi habari mbali mbali, ingawa sayansi na teknolojia inawaweka wanahabari hao katika hali hatarishi, hivyo ipo haja ya kujua jinsi ya kujilinda ili kuwa katika hali ya usalama. "Naamini kwamba baada ya mafunzo haya mtajua namna ya kujilinda, hivyo nawaomba musipende kukaa na watu msiowafahamu na mnapopigiwa simu tuwe makili ili tusije tukaingia katika matatizo", alisema Mjumbe huyo. Kwa upande wake Afisa Program Machapisho, Utafiti na Mafunzo kutoka UTPC Victor Maleko ali...

UBALOZI NORYWAY TAZANIA WAIPONGEZA TAMWA -ZANZIBAR UTEKELEZAJI MRADI WA 'SWIL'

    Na Muhammed Khamis,TAMWA-ZNZ Ubalozi wa Norway Nchini Tanzania umeelezwa kufurahishwa kwake na mafanikio makubwa yalioanza kuonekana katika utekelezaji mradi wa kuinua ushiriki wa wanawake katika uongozi Zanzibar (SWIL)   Mradi huo unaotekelezwa na TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na Asasi nyengine za kiraia ikiwemo ZAFELA na PEGAO na hadi sasa umefikia wananchi wapatao 6917 Unguja na Pemba huku wanawake wakiwa ni  4797 na wanaume 2120.   Wakijadili utekelezaji mradi huo katika ofisi za TAMWA-ZNZ zilizopo Tunguu Wilaya ya kati Unguja maafisa hao wakiongozwa na Bjorn Midthum walisema kuna mengi makubwa yameonekana kwenye mradi huo kwa kipindi cha miaka miwili tangu kuanza kwake mwaka 2020 hadi sasa.   Alisema kuna idadi kubwa ya wanawake wengi zaidi waliojitokeza kugombea na kushinda nafasi tofauti za uongozi kuanzia kwenye vyama vya siasa na asasi za kiraia. Alieleza kuwa mabadiliko hayo yote anaamini yamekuja kutiokana na nguvu kubwa kupitia mradi huo na hat...

KHADIJA HENOCK: DIWANI WADI YA OLE ATAJA YANAYOMKOSESHA RAHA

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA “KUTOKANA malezi mazuri niliyolelewa na wazazi wangu, baada ya kumaliza skuli sikujipweteka… nilianza kazi ya kuisaidia jamii na mpaka sasa naendelea”, …Si maneno ya mtumwengine, bali ni ya Khadija Henock Maziku mkaazi wa shehia ya Mjiniole ambae kwa sasa ndio Diwani wa Wadi ya Ole, Jimbo la Ole wilaya ya Chake chake Pemba. HARAKARI ZA UONGOZI Khadija alianza harakati zake za uongonzi tangu mwaka 2007 akiwa katika Jumuiya ya Wanawake (JUWAKAP). Kwa wakati huo, ambayo ilishirikiana na Shirika la Action Aid, akiwa kama Makamu Mwenyekiti kwa wilaya ya Wete na hatimae kuwa Katibu kwa Mkoa wa Kaskazini Pemba. Dira ya Jumuiya hiyo ilikuwa ni kumkomboa mwanamke, katika nyanja zote za kisiasa, kijamii na kiuchumi. Kazi yao ni kuhamasisha wanawake kugombea nafasi za uongozi, ili waondokane na utegemezi huku wakiwa mstari wa mbele kupiga vita vitendo vya ukatili na udhalilishaji. Mwaka 2009 walifikiwa na mradi wa WEZA kutoka TAMWA, ambao uliwahamasisha...

WATOA HUDUMA ZA MATIBABU WAZALISHA JANGA JIPYA KWA WAGONJWA WANAWAKE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KELELE zinazopigwa na Serikali na jumuiya mbali mbali za kukemea vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa wanawake na watoto, bado wapo wanaotia pamba za masikio.   Cha ajabu na chakusikitisha, wapo hata wazazi na walezi, waalimu na sasa hata kumeibuka wale watoa huduma wa afya, kutajwa katika hilo. Mwaka 2019, kama ilikuwa kisirani kwa watoto na wanawake, kufanyiwa ukatili na udhalilishaji na madaktari kisiwani Pemba. Mfano Novemba 21, mwaka 2019, katika hospitali ya Chake chake, daktari wa kitengo cha Atrasaund, alishikiliwa na ZAECA kwa tuhuma za kuomba rushwa ya ngono kwa mjamzito, kama sharti la kumpa huduma. Kisha kesi hiyo baada ya uchunguzi na kuhojiwa, alifikishwa mahakamani, ingawa Januari 1, mwaka jana aliachiwa huru, kwa sababu mbali mbali zikiwemo ushahidi kutoumuunganisha na kesi Aidha Disemba 18, mwaka 2019, TBC 1 iliripoti Afisa Muuguzi msaidizi wa kituo cha Afya Mamba mkoani Katavi kushikiliwa na Jeshi la Polisi, kwa tuhuma z...