Skip to main content

Posts

UWE KARIBU NASI KWA HABARI NA MATUKIO

'THBUB' YAZINOA TAASISI ZA SMZ PEMBA KUHUSU HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

  TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ofisi ya Zanzibar, imewapa elimu ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora, watumishi kutoka taasisi mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Akizungumza katika mafunzo hayo, huko ukumbi wa Wizara ya Fedha uliopo Gombani, Wilaya ya Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba, Naibu Katibu Mtendaji THBUB, Bw. Juma Msafiri Karibona, aliwaeleza watumishi hao juu ya umuhimu wa kutambua Haki za Binaadamu na misingi ya Utawala Bora. Amesema, lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uelewa mpana watumishi hao ili wawe mabalozi wazuri wa kueneza dhana nzima ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa jamii zao. Aidha, Bw. Karibona alizisitiza suala la ushirikiano baina ya Tume, taasisi za SMZ na wadau wengine wa haki za binadamu ili kuendelea kulinda na kukuza haki za binadamu na misingi ya Utawala Bora. Naye, Afisa Mdhamini Ofisi ya Rais Ikulu, Kisiwani Pemba Bi. Shuweikha Abdalla Omar ameishukuru THBUB kwa kuandaa mafunzo ...
Recent posts

NKURUMAH YAMPA TANO DK. MWINYI KUKIREJESHA TENA CHUO HICHO

    NA HAJI NASSOR @@@@ UONGOZI wa Chuo cha Ualimu Nkurumah Zanzibar, umempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, kwa maono yake ya kitaaluma, yaliosababisha kukirejesha tena chuo hicho.   Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa chuo hicho, Ame Haji Vuai, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi chuoni hapo, kuhusu ufufuaji wa chuo hicho.   Alisema, Dk. Mwinyi amekuwa na maono ya mbali kwenye sekta kadhaa, ikiwemo taaluma, na sasa tayari chuo hicho, kinatimiza miaka mwili tokea, kulipozinduliwa tena mwishoni mwa mwaka jana.   Alieleza kuwa, kwa sasa chuo hicho, kinayo majengo mapya na ya kisasa yenye vifaa na vitendea kazi vya kisasa, chini ya mtaala mpya.   ‘’Kwa hakika Dk. Mwinyi ni kiongozi mahiri na mpenda taaluma, na hasa eneo la kuongeza idadi ya waalimu, tena wale ambao watakwenda kuwasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum,’’alifafanua.   Aidha Mkuu huyo wa chuo, alisema baada...

‘RESI’ ZA NGALAWA MANAHOZA WAMBAA, MAKOMBENI, MAKOONGWE WAZAA 'DABI'

    NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@ NGALAWA ni usafiri ambao wazee wa zamani, waliutumia kwa ajili ya safari zao, hasa kwa shughuli za kibiashara na uvuvi. Usafiri huu ni urithi wa utamaduni wa mzanzibari, ulioanza kutumika katika miongo iliopita, ingawa hadi sasa hutumiwa, lakini sio sana kama ilivyokua hapo zamani. Hili limepelekea kuchukuliwa kama moja ya urithi mkubwa wa kihistoria kwa waswahili wa Zanzibar na wale wa ukanda wa pwani. Ndio maana, katika matamasha mbalimbali ya utamaduni wa Zanzibar, ngalawa zimekua sehemu muhimu ya matamasha hayo na kua kivutio kikubwa kwa hadhira. Kwani hadhira kubwa ya watu ambao huenda katika matamasha hayo, hufurahia kuona jinsi watu wanavyoendeleza utamaduni huo, ambapo huko hufanyika mashindano ya resi za ngalawa. Septemba 21, mwaka huu ilikuwa ni siku ya pili ya tamasha la 31 la utamaduni wa mzanzibari, tokea kufunguliwa kwake Septemba 19, ilikua ni siku ya kukumbuka urithi wa utamaduni wa kuendesha ngalawa. Utamaduni a...

MCHEZO WA NG’OMBE PEMBA, UTAMADUNI UNAOBEBA WASHABIKI WINGI

                                  NA MARYAM SALUM, PEMBA@@@@   KELELE za watazamaji, mlio ya zumari, ukichombozwa na ngoma za asili, ndizo zinazoteka nyonyo za wapenzi wingi wa mchezo wa Ng’ombe, baada ya mpira wa miguu.   Mchezo huu ambao umejengeka katika historia ya   maisha ya jamii ya Pemba, si burudani pekee, bali ni sehemu ya urithi wa kitamaduni unaounganisha vizazi vya zamani sasa.   Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali kuhusu historia ya mchezo huo, asili yake Pemba imehusishwa na mwingiliano wa kihistoria, kati ya jamii za Pemba na Wareno.     Baadhi ya vyanzo vinaeleza kuwa, mchezo huo uliingia katika visiwa hivyo kupitia Wareno, ingawa simulizi za wenyeji pia, zimekuwa zikihifadhi historia yake, kutoka kizazi hadi kizazi.   Akizungumza, katika mchezo wa Ng’ombe uliofanyika uwanja cha Pujini wilaya ya Mkoani, Wazir...

TASFAM: A FIVE- YEAR PROJECT THAT WILL TRANSITION PEMBA FROM THE THEORY OF THE BLUE ECONOMY TO ACTION

    BY MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@ PEMBA Island is among the areas that rely heavily on marine resources to boost the economy of its citizens. For centuries, the ocean has been a source of food, employment, income, and trade for its residents. However, climate change, unsustainable fishing, and economic challenges have been threatening the stability of this crucial sector. In addressing these challenges, the Revolutionary Government of Zanzibar—through the Ministry of Blue Economy and Fisheries, in collaboration with the World Bank—has introduced the TASFAM project. WHAT IS TASFAM? It is the Sustainable Marine Fisheries and Aquaculture Management Project (Tanzania Scaling-up Sustainable Marine Fisheries and Aquaculture Management). This is a five-year project (2025–2030) signed on September 3, 2025, with implementation starting on December 3, 2025, and expected to end on June 30, 2030. According to the Assistant Coordinator of TASFAM in Pemba, Dr. Hamad Maalim Sh...