KHAULAT SULEIMAN, PEMBA@@@@ MKAGUZI wa Polisi Inspekta Khalfan Ali Ussi, amewataka wazee wa watoto wenye ulemavu wa ualbino kisiwani Pemba, kutojiweka pembeni katika kusimamia malezi ya watoto wao. Alisema kuwa jeshi la polisi, limeanda mpango maalumu wa kuwasajili watu wenye ulemavu ualbino Tanzania nzima, ili kuweza kufuatilia na kubaini changamoto zinazowakabili. Aliyasema hayo katika skuli ya Pandani mkoa wa kaskazini Pemba, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kutembelea na kusikiliza changamoto mbali mbali, zinazo wakabili makundi maalum katika shehia ya Pandani. Aidha alisema kuwa jeshi la polisi limeweka mikakati madhubuti wa kuhakikisha usalama kwani jeshi hilo linahakikisha linalinda raia na mali zao. "Wananchi ondoweni hofu na kuishi kwa amani, kwani nyinyi ni raia wema wenye haki sawa na wingine,’’alisema Mkaguzi huyo. Hata hivyo, amewakumbusha wazazi na walezio hao, kuhakikisha watoto hao wanapatia haki zao zote...