NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@ MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar Othman Massoud Othman, amesema Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, ndio yaliotengeneza mwanga, na kisha kufungua milango ya fursa sawa kwa wote, ikiwemo elimu bila ya ubaguzi. Alisema, Mapinduzi hayo ndio yaliyojenga ngome ya uhakika kwa kila mzanzibari, katika kupata elimu, matibabu na huduma nyingine za kijamii bila ya ubaguzi wowote. Makamu huyo wa Kwanza, aliyasema hayo leo Disemba 30, 2023 Kisiwa cha Kojani wilaya ya Wete Pemba, mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la skuli ya ghorofa ya msingi ya Kojani, ikiwa ni shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Alisema, ujenzi wa skuli hiyo pamoja na nyingine, ni mkakati endelevu wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, wa kuhakikisha inawapatia wananchi wake haki ya elimu, waliyoikosa kabla ya Mapinduzi. Alieleza kuwa, elimu ndio msingi wa uhakika wa maendeleo ya mwanadamu, na ndio maana hata Muumba katika kuwaumba wanaadamu, kuliambatana na tendo la kupe