NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ KITUO cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ sasa kimeelekeza nguvu yake kwa wananchi wa shehia ya Wingwi Mjananza wilaya ya Wete Pemba, kwa kambi ya siku tatu, ya kutoa elimu, ushauri na msaada wa sheria bila ya malipo. Kambi hiyo, ipo ndani ya skuli ya Msingi ya Mjananza, ambayo ilianza jana April, 16, na ikitarajiwa kumalizika kesho majira ya saa 8:15 jioni. Akizungumza na wananchi hao, juu ya utaratibu wa utoaji wa msaada huo, leo April 17, 2025 skulini hapo, Afisa Miradi wa ‘ZLSC’ Beny Louis Mlingi, alisema kwanza, mwananchi atapaswa asajiliwe, kwenye fomu maalum kambini hapo. Alieleza kuwa, baada ya hapo atakutana na wanasheria nguli pamoja na mawakili na Vakili , wanaofanyakazi Kituo cha Huduma za Sheria, kwa ajili ya kusikilizwa lalamiko lake. Alifahamisha kuwa, katika kambi hiyo, inawakaribisha wananchi wenye changamoto za kisheria, kama vile migogoro ya mipaka, ardhi, matunzo kwa watoto, waliokosa vyeti vya ndoa, vya kuzaliwa. Eneo j...