NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa shehia ya Shungi wilaya ya Chake chake Pemba, wameikumbusha serikali, kuwajengea barabara yao ya Chanjamjawiri- Tundaua kwa kiwango cha lami, ili wapate kuitumia kwa utulivu. Walisema, kwa sasa imesambaa mashimo na msingi yenye kina kirefu, jambo ambalo haliwapi utulivu, wakati wanapokwenda kwenye shughuli zao za kimaisha. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi shehiani hapo, walisema barabara hiyo ambayo awali ilikuwa na lami, kwa sasa zaidi ya miaka minne imekuwa ikihataraisha waenda kwa miguu, achia mbali wanaotumia vyombo vya moto. Mmoja kati ya wananchi hao Moza Suleiman Mohamed wa Misooni alisema, hasa wao akinamama wamekuwa wakipata usumbufu mara pale wanapokuwa wajawazito. ‘’Hutokezea sisi kutakiwa kuripoti hospitali ya Chake chake kwa huduma na uchunguuzi zaidi, lakini tunapoitumia barabara kutokana na mashimo yaliomo, hupata mtikisiko,’’alieleza. Nae Asma Said Abdalla wa Chanjamjawiri, alisema barabara hiyo ndio wanayoitum