MARYAM THANI: MWAKILISHI ALIEPANIA KUMALIZA CHANGAMOTO KATIKA JIMBO LAKE, Anasema, ataendelea kugombea uongozi kuhakikisha jimbo lake linapata maendeleo zaidi
NA ZUHURA JUMA, P EMBA@@@@ KATIKA jamii inayokuwa kwa kasi, uongozi wa wanawake umekuwa muhimu zaidi kuliko wakati mwengine wowote. Leo tunazungumza na mwakilishi wa Jimbo la Gando wilaya ya Wete kupitia chama cha Mapinduzi CCM, Maryam Thani Juma ambae aliepania kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika jamii. Mwanamama huyo amefanya mambo mengi katika vipindi viwili vya uongozi wake tangu mwaka 2015 hadi sasa ambapo wananchi wa jimbo lake wanannufaika nayo. Maryam ni mwanamke jasiri alieweza kuvuka vikwanzo vingi na hatimae kufanikiwa kuingia kwenye chombo cha maamuzi baada ya kuchaguliwa na wananchi kwa kishindo. Baada ya kuwafikishia wananchi wake maendeleo, ilipofika mwaka 2020 alipoingia tena kwenye kinyang’anyiro cha kugombea, alifanikiwa pia. HARAKATI ZAKE UONGOZI ZILIANZIA WAPI? Mwakilishi huyo alianza uongozi kwenye chama akiwa kama Katibu wa Uchumi na Fedha katika tawi la Kizimbani Wete Pemba, baadae akawa Mjumbe wa Kamati Tekelezaji ya Vijana Wilaya ya Wete kwa wakati hu...