HABIBA ZARALI, PEMBA@@@@ NI majira ya saa 4:00 asubuhi, nilipofika katika bonde la Kigawani kijiji cha Chwale Wilaya ya Wete Pemba, nikitokea Mkoani. Katika safari hiyo niliyochukuwa muda usiopunguwa saa 1:30 kwa usafiri wa umma, nikiwa na lengo la kutaka kujuwa changamoto na maendeleo ya kilimo msitu ambacho kinalimwa shehiani humo. Ilikuwa ni safari yenye kheri kubwa, kwani kukutana na wakulima wa kilimo msitu, ambao wameamuwa kujikita na kilimo hicho wakiwa na malengo ya kujikwamua kimaisha. Pamoja na wakulima wengine kuzungumza nao nilipata hamu na shauku kubwa ya kuzungumza na mkulima Naomba Shaaban Mbarouk, baada ya kumsikia kuwa alikotokea hakuwa na hamu ya kujiingiza katika kilimo hicho. Wala sikufanya ajizi nilimvuta pembeni, chini ya muembe huku upepo ukitupepea taratibu akiielezea makala haya, kinaga ubaga kuhusu kilimo hicho kilichomvutia hadi kujiingiza. Alijiingiza katika kilimo hicho, baada ya kupata mafun...