Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar Riziki Pembe Juma amesema hakuna sababu ya kuendelea na ukiukwaji wa haki za binadamu na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kutokana na mila zenye madhara. Kauli hiyo ameitowa jana wakati wa kufunga mkutano wa kimataifa wa ukeketaji, uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es salaam, amesema hakuna sababu kuendelea na ukiukwaji wa haki za binadamu na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kutokana na mila zenye madhara katika makundi hayo. Aidha amesema mapendekezo yaliyotolewa katika mkutano huo yakitekelezwa vizuri yataokoa na kuwalinda wanawake na wasichana dhidi ya vitendo hivyo viovu katika mataifa mbali mbali. Waziri huyo ametaja baadhi ya mapendekezo yaliyopendekezwa katika mkutano huo ikiwemo ushirikishwaji wa jinsia zote pamoja kuwajengea uwezo wavulana na wasichana kukataa ukeketaji, Tume ya Umoja wa Afrika kuratibu mikutano mikuu pamo...