Kamati ya wataalamu wa masuala ya Habari Zanzibar (ZAMECO) inayoundwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA- Zanzibar), Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA), Jukwaa la Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC Zanzibar) , Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) pamoja na Klabu ya Waandishi wa Habari Pemba (PPC) imelaani video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha wasichana wawili wakirekodiwa na kuulizwa maswali yasio na maadili na yenye kuvunja heshima na haki za binaadamu. Tukio hili limeibua hisia kali kwa wadau wa habari, watetezi wa haki za binaadamu na jamii kwa ujumla na kuibua maswali yasio na majibu miongoni mwa wanahabari kuhusu maadili, haki za binadamu, na misingi ya uhuru wa vyombo vya habari. Hivyo basi ZAMECO inasisitiza kuwa vitendo vya udhalilishaji kwa watoto wa kike na jamii kwa ujumla ni ukiukwaji wa haki za binaadamu, maadili ya uandishi wa habari, na...