NA HAJI NASSOR, ARUSHA RAIS wa Mahkama ya Afrika ya haki za binaadamu na haki za watu Imani Daud Aboud, amesema kama waandishi wa habari wanafanyakazi zao chini ya vitisho kutoka kwa mamlaka kunahatarisha kudhoofisha uhuru wao na ule wa kujieleza na kutoa maoni. Rais huyo aliyasema hayo jana ukumbi wa mahakama hiyo mkoani Arusha alipokuwa akifungua mkutano wa kikanda kwa waandishi wa habari juu ya ulinzi na usalama wao uliondaliwa na Baraza la habari Tanzania MCT. Alisema vipo vyombo au mamlaka vimekuwa vikiingilia na kuwatisha waandishi wa habari wanpokuwa kazini jambo ambalo halisidii kuimarisha uhuru wa kujieleza na ule wa habari. Alieleza kuwa, haki ya kupata na kusambaaza habari ni haki ya kikatiba hivyo ni kosa kwa mamlaka nyingine kuviingilia vyombo vya habari pasi na dai la haki. 'Waandishi wa habari ni sauti ya wsiokuwa na sauti na ni sauti kwa waliokata tamaa hivyo ni jukwaa muhimu na linapaswa lilindwe na sio kushambuliwa,'alieleza. Katika hatua nyingine rais huyo