NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ UONGOZI wa skuli ya sekondari ya Fidel Castro, wananchi kijijini hapo, pamoja na uongozi wa shehia ya Wawi wilaya ya Chake chake, umekubaliana kupiga marufuku kuanzia sasa, kutoingia kwa mtu yeyote bila ya kazi ya halali, ndani ya eneo la skuli, ili kuepusha athari ambazo zimeanza kujitokeza. Wakizungumza kwenye kikao cha pamoja, kilichofanyika skulini hapo, walisema tayari athari kama za wizi wa vifaa vya wanafunzi, umeanza kujitokeza, hivyo wamekubaliana kuanzia sasa kupiga marufuku, uingiaji kiholela. Mwalimu mkuu wa skuli hiyo Seif Hamad, alisema ameridhishwa na uamuzi uliofikiwa na pande mbili hizo, kwani wamekuwa na hofu kubwa ya kutokezea vitendo vya udhalilishaji hapo baadae. Alieleza kuwa, uamuzi huo unaweza kusaidia sana kuondosha uingiaji holela ndani ya skuli hiyo, ambao kwa kiasi kikubwa, ulikuwa unaanza kutishia hata mali za skuli. ‘’Mimi nimeridhishwa na uamuzi ambao umefikiwa kati yetu, wazazi na uongozi wa shehia, kwamba sasa t...