NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ JESHI la Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, limesema haliko tayari kuona maisha ya wavuvi yako hatarini, kwa kule kutofuatilia taarifa za wataalamu wa mamlaka ya hali ya hewa nchini. Hayo yameelezwa bandari ya Tanda Tumbi, kwa nyakati tofauti na Mkaguzi wa shehia ya Mjananza kutoka Jeshi la Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Inspekta Khalfan Ali Ussi, wakati akizungumza na wavuvi hao, kwenye bandari za shehia hiyo, alipofanya ziara maalum. Alisema, Jeshi la Polisi linawajibu wa kuwakumbusha wavuvi hao, kufuatilia kila siku taarifa za utabiri wa hali ya hewa, kwani Jeshi halipendi kuona maisha yao yako hatarini. Alieleza, kuwa, wavuvi ni moja ya kundi lenye thamani kubwa katika jamii, hasa la kukuza pato la taifa, na ndio maana Jeshi la Polisi, likaamua kukutana nao, ili kuwakumbusha jambo hilo. Aidha Inspekta huyo alifahamisha kuwa, hasa kwa kipindi hichi cha kuvuma upepo wenye kasi ya ajabu, ambao unauwez...