Skip to main content

Posts

Showing posts with the label MSAADA KISHERIA

HAROUN AFURAHISHWA SERIKALI KUUNGA MKONO HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA

    NA HAJI NASSOR, ZANZAIBAR@@@@ WAZIRI wa Nchi, Afisi ya Rais, Katiba, Sheria na Utawala Bora Zanzibar Haroun Ali Suleiman, amesema inafurahisha kuona serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zinashirikiana katika kufanikisha utoaji wa msaada wa kisheria. Alisema, ushirikiano huo umesababisha kuimarika kwa utoaji huo wa msaada wa kisheria, ikiwemo kupitia kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. Waziri Haroun aliyasema hayo leo Novemba 20, 2024  ukumbi wa mikutano wa Michezani Mall, wakati akilifungua jukwaa la nne la msaada wa kisheria, lililoandaliwa na Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar, kwa ushirikiano na UNDP. Alisema, kwa upande wa Zanzibar Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi amekuwa mstari wa mbele, kuungano mkono utoaji wa msaada wa kisheria, ikiwemo kutoa bajaji saba, kwa watoa msaada wa kisheria Zanzibar. Alieleza kuwa, hili ni jambo la kupongezwa, kwa vion...