NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ SIKU hizi imekua tofauti na zamani, wanawake kuwa viongozi sio jambo geni kujitokeza kugombea nafasi hizo na kushinda. Nchi kadhaa, hivi sasa zimeendelea kutokana na wanawake kupewa nafasi za uongozi na kufanikiwa kuleta mabadiliko ya kiutendaji. Mataifa kama ya Ethiopia, Liberia pamoja na Tanzania, ambazo uchumi wake umepanda na kupata mabadiliko makubwa katika sekta tofauti. Ellen Johnson-Sirleaf ni Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika, hata hivyo yeye sio mwanamke wa kwanza kuongoza nchi barani Afrika. Maana yupo Malikia Zauditu wa Ethiopia alieongoza nchi yake kwa miaka 13 toka mwaka 1917 hadi 1930. Katika miaka michache iliopita, Tanzania imepata mafanikio makubwa, ikiwa pamoja na utulivu wa kisiasa na maendeleo katika sekta mbali mbali kufuatia uongozi wa nchi kushikwa na Rais wa kwanza mwanamke, Dk. Samia Suluhu Hassan. Mama Samia hivi sasa anahesabika kuwa ni mfano mzuri wa kuigwa na wanawake wa h...