NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ KAMATI ya maadili na taaluma ya shehia za Wambaa na Chumbageni wilaya ya Mkoani Pemba, imepiga marufuku kufanyika vitendo viovu, vinavyofanywa na baadhi ya vijana, katika ya fukwe ya bandari ya Kwakitunga Wambaa. Kamati hiyo imesema, wamebaini kuwa, kila ifikapo siku za sikukuu na mwishoni mwa wiki, wapo vijana, wengi wao kutoka nje ya shehia hizo, huitumia fukwe hiyo, kwa kufanya mambo machafu. Akizungumza kwenye kongamano la malezi na maadili, lililofanyika Wambaa sokoni, Mjumbe wa kamati hiyo sheikhe Mahamoud Hussein, alisema hawakatai vijana kusherehekea sikukuu, bali wanachopiga marufuku ni uvunjifu wa maadili. Alisema, suala la furaha ni jambo jema, baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhan, ingawa wanachokipinga ni kufanyikwa vitendo vya udhalilishaji. Alieleza kuwa, uislamu haukatazi furaha kwa mtu yeyote, bali kinachotakiwa iwe ni kwa kufuata maadili na misingi ya dini ya kiislamu, ili furaha hiyo isigeuke nakama. āāKama...