NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ KATIBU wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, amesema tayari serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imeanza kwa vitendo kukifungua kisiwa cha Pemba kiuchumi. Mhandisi Zena aliyasema hayo jana, eneo huru la Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba, mara baada ya kuyapokea matembezi ya wanavikundi vya mazoezi na wananchi, kwenye kongamano la uwekezaji la mwaka 2025, yalioandaliwa na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar ‘ZIPA’. Alisema, kufanyika kwa kongamano hilo ni sehemu ya kukifungua kisiwa hicho kiuchumi, ujenzi wa barabara kadhaa za kisasa pamoja na utanuzi na ujenzi wa bandari mbali mbali. Alisema, serikali inayoongozwa na Dk. Hussein Ali Mwinyi, inaendelea kuonyesha kwa vitendo nia yake ya kukifungua kisiwa cha Pemba, kama alivyokuwa akiinadi wakati wakati wa kampeni. Alieleza kuwa, kilichobakia kwa wananchi wa Pemba, ni kushirikiana kwa karibu na serikali yao, ambayo ina nia ya dhati kuona uchumi wa Pemba, u...