Na, Hassan Msellem, Pemba. MAHAKAMA ya Mkoa Chake Chake, imemuhukumu kutumia chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka 15 Ali Ussi Simai mwenye umri miaka 25 mkaazi wa shehia ya Mchakwe wilaya ya Mkoani ambae ni maalim wa madrasa, baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi wake, mwenye miaka minane (8). Hukumu hiyo imetolewa jana Mei 18, mwaka 2022 na hakim Muumin Ali Juma wa mahakama ya Maalum ya makosa udhalilishaji, katika Mahakama ya mkoa Chake Chake. Awali ilielezwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka wa Serikali Ali Amour Makame kuwa mshtakiwa huyo, alitenda kosa hilo Novemba 28 mwaka 2021 majira ya saa 9:pp jioni huko Mchakwe Mwambe Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba. Mshitakiwa alikuwa na mashahidi wa tatu ambao ni wanafunzi wawili ambao wote ni wanafunzi wake wa madrassa pamoja na mshitakiwa mwenyewe ambao walitoa ushahidi wa kupinga Mwalimu huyo kutenda kosa hilo. Kwa upande wa mashtaka iliwa na mashahidi watano ambao ni mtoto mwenyewe aliefanyiwa kitendo hicho cha ubakaji, Daktari aliemfanyia vipimo, wazazi wake pamoja na Askari wa upepelezi ambao walitoa ushahidi wao mahakamani hapo ambao ulitosha kumtia hatiani mshitakiwa huyo. Ndipo hakimu Muumin Ali Juma bila ya kuwa na chembe ya shaka kutokana na ushahidi uliotolewa alikubaliana na upande wa mashtaka na kumuamuru mshitakiwa Ali Ussi Simai kutumikia Chuo cha mafunzo kwa kipindi ch miaka 15 ili iwe fundisho kwake na kwa wengine wenye tabia kama hiyo. Mwisho.
|
Comments
Post a Comment