Skip to main content

MCT LATANGAAZA MAJINA WASHINDI TUZO ZA WANAHABARI: ZANZIBAR LEO PEMBA WAUPIGA MWINGI

 



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 Dar es Salaam, Alhamisi, Mei 19, 2022

Jopo la majaji saba lililokaa kwa siku tisa, kuanzia Mei 7 hadi 15, 2022 kupitia jumla ya kazi 598 za waandishi zilizokuwa katika makundi 20 ya kushindaniwa katika Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2021, limemaliza kazi yake, Mei 15, 2022.

 

Jopo hilo lilitumia siku tisa badala ya nane kutokana na ongezeko la kazi 202 kutoka Tuzo za EJAT 2020, ambapo jumla ya kazi 396 ziliwasilishwa ukilinganisha na kazi 598 za sasa. Hapa niwapongeze na kuwashukuru majaji kwa kazi kubwa waliyoifanya usiku na mchana yakupitia kazi hizo.

 

Jopo liliongozwa na mwenyekiti, Mkumbwa Ally. Wajumbe wengine walikuwa Mwanzo Millinga (Katibu), Aboubakar Famau, Mbaraka Islam, Imane Duwe, Beatrice Bandawe, na Rose Haji, ambao waliapishwa Mei 6, 2022 na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jaji Robert Makaramba.

 

Majaji hao wameteua jumla ya waandishi 60 ambao kazi zao zimeonekana kuwa bora Zaidi na ambao miongoni mwao watapatikana washindi wa EJAT 2021.  Kati ya wateule hao, wateule tisa wanaandikia runinga; 12 vyombo vya mtandaoni, wanane redio na 31 wanaandikia magazeti.

           

Idadi ya wateule wa EJAT 2021 kwa upande wa wanawake ni 28 ambayo ni asilimia 47 ikiwa ni ongezeko la asilimia tatu kulinganisha na Tuzo zilizopita ambapo wanawake walikuwa 26 sawa na asilimia 44 ya walioingia kwenye hatua hii mwaka jana. Wateule wanaume ni 32, sawa na asilimia 53.

 

Kati ya wateule 28 wanawake, 18 wanatoka katika magezeti, runinga wametoka watatu, radio wawili na vyombo vya habari vya mtandaoni watano. Kwa upande wa waandishi wa habari wanaume, magazeti wametoka 12, runinga waandishi sita, radio wateule sita na vyombo vya habari vya mtandaoni wateule saba.

 

Kwa mujibu wa majaji wa EJAT 2021, kazi za mwaka huu, zimeonyesha kuwa na kiwango cha juu ukilinganisha na mwaka jana. Hii ni pamoja na kiwango cha waandishi wa habari wa vyombo vya mtandaoni kuonyesha kukomaa zaidi katika kazi zao na mwamko wa ushiriki katika Tuzo hizo.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi katika shughuli za utoaji Tuzo na ndiye atakaye mkabidhi Tuzo mshindi wa jumla pamoja na mshindi wa Tuzo ya Maisha ya Mafanikio Katika Uandishi wa Habari  (LAJA) 2022.

 

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Mei 28, 2022 katika ukumbi wa Hoteli ya Serena, Dar es Salaam. Hii itakuwa ni mara  ya 13 kuwatuza waandishi waliofanya vizuri katika kazi zao za kiuandishi katika mwaka uliotangulia.

 



Baraza linapenda kuwataarifu waandishi wa habari kuwa katika Tuzo za mwakani, mfumo wa ujazaji fomu utakuwa ni kwa njia ya mtandao (online) ambapo fomu zitajazwa na kutumwa kwa mtandao. Hii itapunguza matumizi ya karatasi na changamoto za CD kukwama kucheza wakati majaji wanapitia kazi.

 

Taasisi zinaounda Kamati ya Maandalizi ni pamoja na MCT, Wakfu wa Vyombo vya Habari (TMF), Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Jukwaa la Wahariri (TEF), HakiElimu, Agriculture Non-State Actors Forum (ANSAF), Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Misa-Tan na Twaweza.

 

Tuzo hizi zinafadhiliwa na Wajibu Institute, Natural Resources Governance Institute (NRGI), Bank ABC, Hakielimu, Tume ya Ushirika, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Busota Inn, Serena Hotel Dar es Salaam, Coca Cola, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Azam Media, Twaweza na COSTECH.

 

Makundi yanayoshindaniwa katika Tuzo za EJAT 2021 ni:-

 

1.                  Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchumi, Biashara na Fedha;

2.                  Tuzo ya Uandishi wa Habari za Michezo na Utamaduni;

3.                  Tuzo ya Uandishi wa Habari za Kilimo na Biashara ya Kilimo;

4.                  Tuzo ya Uandishi wa Habari za Elimu;

5.                  Tuzo ya Uandishi wa Habari za Utalii na Uhifadhi;

6.                  Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchunguzi;

7.                  Tuzo za Uandishi wa Habari za Data;

8.                  Tuzo za Uandishi wa Habari za Haki za Binadamu

9.                  Tuzo za Uandishi wa Habari za Utawala Bora na Uwajibikaji;

10.              Mpiga Picha Bora – Magazeti;

11.              Mpiga Picha Bora – Runinga;

12.              Mchora Katuni Bora;

13.              Tuzo ya Uandishi wa Habari za Jinsia na Watoto;

14.              Tuzo ya Uandishi wa Habari za Gesi, Mafuta na Uchimbaji Madini;

15.              Tuzo za Uandishi wa Habari za Walemavu;

16.              Tuzo za Uandishi wa Habari za Afya;

17.              Tuzo ya Uandishi wa Sayansi na Teknolojia;

18.              Tuzo za Uandishi wa Habari za Hedhi Salama;

19.              Tuzo za Uandishi wa Habari za Ushirika; na

20.              Kundi la Wazi.

 

Ifuatayo ni orodha ya wateule wa EJAT 2021 pamoja na vyombo vyao:  

 

SN

NOMINEES

MEDIA OUTLETS

1

Mariam Shabani Mbwana

Mwananchi

2

Tumaini Godwin Msowoya

Mwananchi

3

Peter Simon Rodgers

ITV

4

Agusta Mathias Njonji

Nipashe

5

Nusra Shaaban Kichongapishi

TIFU TV- Online

6

Adam Gabriel Hhando

CG FM Radio

7

Haji Nassor Mohamed

Zanzibar Leo

8

Khamisuu Abdallah Ali

Zanzibar Leo

9

Naishooki Alais Makaseni

STAR TV

10

Sanula Renatus Athanas

Nipashe

11

Lugendo Ibrahim Madege

UFM Radio

12

Anthony Mayunga Mayunga

Mwananchi

13

Ephrahim Edward Bahemu

Mwananchi

14

Maryam Salum Habib

Zanzibar Leo

15

Said Seleman Lufune

City FM

16

Pascal Michael Buyaga

TBC1

17

Aurea Simtoe

Mwananchi

18

Salum Vuai Issa

Zanzibar Leo

19

Masekepa Natisa Masekepa

ITV

20

Sabato Mafwiri Kasika

Nipashe

21

Muhidin Ally Msamba

The Guardian

22

Amina Ahmed Mohamed

Zanzibar Leo

23

Harith Jaha Ally

Watetezi TV - Online

24

Gladness Joseph Msetti

UFM RADIO

25

Zuhura Hassan Makuka

Dar 24 (Online)

26

Jackline Inyas Silemu

ITV

27

Francis Dhamira Kajubi

The Guardian

28

Isakwisa Njole Mbyale

Highlands FM radio

29

Harieth Isaya Makweta

Mwananchi

30

Halfan Chusi

Nipashe

31

Khalifa Said Rashid

The Chanzo – Online

32

Irene Nicholaus Mwasomola

Uhuru

33

Elizabeth Edward Kusekwa

Mwananchi

34

Baraka Jailos Messa

Habari Leo

35

Martha Stephen Nalimi

Shamba FM

36

Joyce David Joliga

The Citizen

37

Mariam Ngollo John

Nukta.blog

38

Najjat Haji Omar

The Chanzo - Online

39

Salma Msichoke Mrisho

STAR TV

40

Peter Lugendo John

TBC FM

41

Beatrice Philemon Mukocho

The Guardian

42

Joe Beda Rupia

Jamhuri

43

Hanifa Salim Mohamed

Zanzibar Leo

44

Amour Khamis Ali

Zanzibar Cable TV

45

Abdi Juma Seleman

Zanzibar Leo

46

Protte Profit Mmanga

LEO TV – Online

47

Faraja John Sendegeya

Azam TV

48

Festo Charles Lumwe

Dar 24 – Online

49

Mary Geofrey Mashina

Nipashe

50

Munira Abdillah Hussein

BBC Swahili (Online)

51

Daniel Samson

Nukta.habari blog

52

Habiba Zarali Rukuni

Zanzibar Leo

53

Marco Zephania Maduhu

Nipashe

54

Christina Stephen Mwakangale

The Guardian

55

Elizabeth Cornery Zaya

Nipashe

56

Sudi Shaban Ally

STAR TV

57

Omary Hussein Omary

STAR TV

58

Jecha Simai Jecha

ZBC FM

59

Jenifer Julius Gilla

The Guardian

60

Lukelo Francis Haule

The Chanzo- Online

 

 

 

 

--------------------------------

Kajubi D. Mukajanga 

Mwenyekiti

Kamati ya Maandalizi ya EJAT 2021

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 mchan

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’’ali

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo ni vy

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa ufafan