NA HAJI NASSOR, PEMBA
MAHAKAMA ya Mkoa Wete, imelazimika
kumlaza rumande kwa muda wa wiki mbili, daktari Is-haka Rashid Hadid, akidaiwa kutenda
makosa manne kwa mtoto mmoja mwenye miaka 16, likiwemo la kumbaka mara tatu.
Akisoma hati
ya mashtaka, Mwendesha Mashtaka kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Juma
Mussa, alidai kuwa, mtuhumiwa huyo
alimbaka mtoto huyo ambae yuko chini ya uangalizi wa wazazi wake.
Alidai kuwa,
baina ya Aprili 21, mwaka huu mtuhumiwa huyo alimtorosha mtoto huyo, kutoka
nyumbani kwao Gombani wilaya ya Chake chake mkoa wa kusini Pemba na kumpeleka nyumbani
kwake Kangagani wilaya ya Wete.
Ambapo baada ya kumtorosha, usiku wake alianza kumbaka na kuendelea kumfanyia kitendo
hicho kwa siku tatu tofauti.
‘’Mtuhumiwa
umetenda makosa manne, kwa mtoto mwenye miaka 16, moja ni kumtorosha na pili
ulimbaka mara tatu, wakati ukiwa nyumbani kwako, eneo la Kangagani wilaya ya
Wete mkoa wa kaskazini Pemba,’’alidai.
Mara baada
ya kusomewa mashtaka yake, mtuhumiwa huyo chini ya wakili wake Abeid Mussa, aliulizwa
na Hakimu wa makosa ya udhalilishaji Ali Abdur-haman Ali, ikiwa anakubali ama
laa.
‘’Umeyaskia
makosa yako vyema, kama yalivyosomwa na Mwendesha mashtaka, kama jawabu ndio
unakubali ama unakataa,’’alimuuliza mtuhumiwa Hakimu huyo.
Mtuhumiwa huyo
alikana tuhuma hizo, na kuiomba mahkama hiyo kumpa dhama kwa masharti nafuu,
ombi ambalo halikuzingatiwa mahakamani hapo.
Hakimu wa
mahkama hiyo, aliliahirisha shauri hilo hadi Juni 1, mwaka huu, na mtuhumiwa
amepelekwa rumande.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, mtuhumiwa
huyo Is-haka Rashid Hadid miaka 27, April 21 mwaka huu, majira ya saa 8:30
mchana, alimtorosha mtoto mwenye miaka 16, kutoka nyumbani kwao Gombani na
kumpeleka nyumbani kwake Kagangani.
Kufanya
hivyo ni kosa kinyume na kifungu cha 113 (1) (a) cha sheria ya Adhabu nambari 6
ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.
Kosa la pili
kwa mtuhumiwa huyo baada ya kumtorosha mtoto huyo, siku hiyo hiyo majira ya saa
3:00 usiku alimbaka, ambapo ni kinyume na kifungu cha 108 (1), (2), (e) na 109
(1) cha sheria ya Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018.
Kosa la tatu
ambalo lilitokea Aprili 22 na la nne ambalo lilitokea Aprili 23, mwaka huu pia,
alilitenda kwa nyakati tofauti za usiku, ambapo alidaiwa kumbaka mtoto huyo.
Ambapo pia
kufanya hivyo, ni kinyume na kifungu cha 108 (1), (2), (e) na 109 (1) cha
sheria ya Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.
Mwisho
Comments
Post a Comment