NA HAJI NASSOR, PEMBA
BAADA ya Jeshi la Polisi mkoa wa
kaskazini Pemba, kumuachia kwa dhamana, daktari Is-haka Rashid Hadid wa kituo
cha afya Gombani Chake chake, anayetuhumiwa kumbaka mgonjwa wake ambae ni
mtoto, hatimea mtuhumiwa huyo amekamatwa tena.
Taarifa
zinaeleza kuwa, daktari huyo aliachiwa kwa dhamana ya Polisi baina ya Mei 5 na
Mei 6 mwaka huu, na baadhi ya wanaharakati wa haki za wanawake na watoto kulitupia
lawama nzito Jeshi hilo.
Walidai kuwa,
lililofanyika ni uzembe ndani ya Jeshi la Polisi, hata kama ikiwa mtoto,
aliyebakwa na daktari huyo aliwataja watuhumiwa wawili tofauti.
Walisema
wanavyofahamu wao, yapo makosa yalioorodheshwa kwenye sheria, kuwa hayana
dhamana likiwemo la ubakaji, ingawa Polisi kaskazini Pemba, wanadai walipingana
na sheria hiyo.
Kwa wakati
huo, wanaharakati hao akiwemo Mkuu wa Idara ya Ustawi wa Jamii wilaya ya Wete,
Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA- Zanzibar walishangaazwa
na kitendo cha daktari huyo, kupewa dhamana.
Kamanda wa
Polisi Mkoani humo Juma Saadi Khamis, alithibitisha kuwa, wamemkamata tena
mtuhumiwa huyo, na wanaendelea na taratibu za kumfikisha mahamamani.
Alisema, ni
kweli mtuhumiwa huyo ambae ni daktari, walilazimika kumuachia kwa dhamana ya
kipolisi, kutokana na mtoto kuwachanganya, juu ya idadi ya watuhumiwa aliodai
kumbaka.
‘’Ni kweli
yule daktari ambae tulimuachia kwa dhamana wiki iliyopita, sasa tumeshamkamata tena
na wakati wowote atafikishwa mahakamani, kujibu tuhuma
zinazomkabili,’’alieleza.
Kamanda huyo
alisema, tayari wameshakamilisha hatua za kumuhoji na wakati wowote, jalada
lake litafikishwa kwa Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, kwa hatua nyingine.
‘’Kwa wakati
ule ni kweli, tulimpa dhamana kwa sababu maalum, na tulimueleza kuwa
tukimuhitaji tutamuita na wakati huo umefika na sasa, tunae kwa ajili ya
kumfikisha mahakamani,’’alifafanua.
Kuanzia
Mei 1 mwaka huu, Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, lililazimika
kumshikilia daktari huyo, kwa tuhuma za kumbaka mgonjwa wake ambae ni mtoto.
Kisha baina ya Mei 5 na Mei 6 mwaka
huu, mtuhumiwa alipata dhamana ya polisi, kwa madai ya mtoto huyo, kutaja watu
wawili tofauti.
Ambapo Kamanda wa Polisi, alisema
walilazimika kumpa dhamana daktari huyo, hadi hapo atakapopatikana mtuhumiwa
mwengine.
Awali mtoto huyo aliyefanyiwa kitendo
hicho alidai kuwa, Aprili 21 mwaka huu, alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa
ajili ya matibabu, na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba
nambari yake ya simu.
Alisema ilipofika usiku, walikuwa
wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms), kwa lengo la kwenda kuchukua dawa
nyingine ambazo kwa mchana huo, alizikosa hospitalini hapo.
"Nilikwenda hospitali
kutibiwa, baada ya kufanya mapele sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka
aje daktari mwengine, kwa hiyo kesho (siku ya pili yake), atakuja kunichukua,
ili ukanipe dawa nyingine", alisema mtoto.
Alidai kuwa, kisha alimchukua hadi
kijiji cha Kangagani wilaya ya Wete, na kumfungia kwa siku tano, na kabla ya
kumbaka alimchunguza virusi vya Ukimwi.
Tukio linalofafana na hilo, liliwahi kutokea Novemba 21, mwaka 2019,
hospitali ya Chake chake, baada ya daktari wa kitengo cha Atrasaund, kudaiwa
kuomba rushwa ya ngono kwa mjamzito, kama sharti la kumpa huduma.
Aidha Disemba 18, mwaka mwaka 2019, TBC 1, iliripoti Afisa Muuguzi
msaidizi wa kituo cha Afya Mamba mkoani Katavi kushikiliwa na Jeshi la Polisi,
kwa tuhuma za kumbaka mjamzito, wakati alipokuwa akimsaidia kujifungua.
Mwisho
Comments
Post a Comment