NA HAJI NASSOR, PEMBA
TANZANIA
imejaaliwa kuwa na vivutio mbali mbali vya utalii.
Vipo vivutio vya Serikali na vivutio vya jamii, vyote vikiwa na jukumu
la kutangaza utalii wa Tanzania.
Miongoni mwa vivutio hivyo ni Mlima wa Kilimanjaro, hifadhi ya wanyama
Serengeti, Tarangire, Burunge, Ngorongoro, pamoja na maeneo mengine ambayo
watalii wanafika.
Hifadhi zote hizo zimekua ni chachu ya maendeleo kwa wananchi
waliozunguka hifadhi hiyo, pamoja na taifa kwa ujumla katika kunufaika.
Moja ya hifadhi ambayo wananchi wamekuwa wakinufaika nayo kwa asilimia
100 ni hifadhi ya jamii Burunge ‘WMA’ iliyopo Babati Mkoani Manyara.
Wananchi wananufaika na hifadhii hii, kupitia hifadhi ya wanayama na
Ziwa burunge, watalii wengi wamekuwa wakimiminika kutembelea hifadhi hiyo
pamoja na kuangalia mafanikio ya ziwa hilo.
Hifadhi ya Burunge imezungukwa na vijiji 10 ikiwemo Sangaiwe, Mwada,
Ngolei, Vilima vitatu, Kokoi, Minjingu na baadhi ya vijiji vyengine.
WANANCHI WANASEMAJE JUU YA UHIFADHI
Venust Peter wa Sangaiwe, amesema sekta ya uhifadhi ya wanyama kijiji
kwao, imekua ni muhimu kabla ya WMA wanapotaka kufanya kitu kijiji hapo, lazima
kuchangishana fedha na kiwango hakipatikani kwani wengine hukimbia kaya zao.
Sasa shuhuli zote za ujenzi hutolewa tenda na watu hupata pesa na
mradi kukamilishwa kwa wakati na wananchi hawasumbuliwi tena kuchangia.
“Uhifadhi umetupatia kipato katika kijiji chetu, baada ya elimu
tunalima na tunaendelea kuhifadhi wanyamapori, tulikua vijiji vitano sasa
vimekua vijiji 10,”amesema.
Stellm Thomas (57) amesema kabla ya uhifadhi ilikuwa ni shida kijijini
kwao, kila ujenzi unakaribia lazima kila kaya kuchangishwa shilingi 20,000 sasa
imekua ni tafauti na huku vijiji vya jirani vikitamani kunufaika nao.
Kwa sasa hata watoto wanapata chakula skuli na matunda, kutoka katika
hifadhi hiyo hii, hali inayowafanya kusoma kwa umakini sasa.
Hifadhi imeweza kujenga shule, vyumba vya kusomea wanafunzi na hata
zahanati kijijini Sangaiwe.
Aambapo wajawazito wanajifungulia hapa na wahatembei tena umbali wa
kilomita 8 kufuata kituo cha afya.
“Mimi natamani sasa nirudi katika ujana wangu, tulikua tunaenda zaidi
ya kilomita 8 kufuata huduma za afya, sasa skuli ipo, zahanati ipo kijijini kila kitu kipo
sawa,”anasema.
Anastazia John Mwanso, anaeleza uhuifadhi umetusaidia kuanzisha vikoba
kwa akinamama, ambapo wanakopeshana na baadhi yao wanafanya biashara ndogo
ndogo.
UWEPO WA KAMERA WANANCHI WANASEMAJE KATIKA HIFADHI
Wanasema utasaidia wakulima wanaozunguka hifadhi, kupata mazao yao,
mbayo walikuwa wakiyakosa kutokana na kuvamiwa na wanyama.
Kamera zitawekwa katika maeneo maamulu, ambayo wanyama wanapita na
kuingia katika mashamba ya wakulima, wataweza kuonekana moja kwa moja na
walinzi kwenda kumfurusha.
Emelda Patrick Sangu (49), amesema uwepo wa kamera umepelekea kuwapa
matumaini makubwa wakulima wengi wanaozunguka hifadhi hiyo ya burunge.
“Uwekaji huo utaambatana na ujengaji wa vibanda pembezoni mwa hifadhi,
kwa jili ya walinzi na kuweza kuwafurusha wanyama,’’anasema.
Mwanakijiji Mofulu Sangawa John (33), anasema licha ya mfumo huo
kuchelewa kuwafika katika kijiji chao, wakulima wamekuwa na mategemeo makubwa,
katika msimu huu kupata mazao mengi.
Kamera hizo zina uwezo wa kumurika umbali wa mita 100, sawa na wanja
wa mpira wa miguu, na zitaweza kutoa taarifa mapema, iwapo kuna wanyama
wanakaribia kuvuka eneo la hifadhi.
KAMATI YA JAMII INAZUGUMZIAJE JUU YA UHIFADHI
Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii Singaiwe Nikodemas Mofulu,
amesema wananchi wanajivunia uhifadhi walionao baada ya elimu waliopatiwa.
Ambapo sasa wanapata fedha nyingi kufuatia kutunza eneo la hifadhi ya
jamii, kwa ajili ya maendeleo yao.
Kwa sasa wamekua na hoteli za kigeni mbili na wanapata shilingi milioni
48 kwa mwaka, hali inayopelekea kupunguza shida ya masafa marefu ya watoto
kufuata huduma za kijamii.
“Kwa sasa
hakuna kutembea zaidi ya kilo mita nane (8), kufuata zahanati vijiji vya
jirani, watoto nao kuacha kuhatarisha maisha yao kwa ajili ya kufuata elimu,’’anasema.
VIONGOZI WA HIFADHI YA BURUNGE WANASEMAJE
Katibu wa ‘WMA’ hifadhi ya Jamii Burunge Benson Mwaise, anasema, wananchi wananufaika na ‘WMA’
kwa kutegemea kupata maji na watalii, hufurahia muonekano wake.
Alivitaja baadhi ya vijiji
zinavyonufaika ni pamoja na Sangaiwe, Mwada, Ngolei na Vilima vitatu, ambapo wamesaidiwa
kupata huduma mbali mbali ikiwemo skuli, zahanati hata watoto kupikiwa chakula
wanapokuwa masomoni.
Msaada mwengine wanafunzi kupatiwa usafiri wa basi, kutoka katika
kijiji chao kwenda na kurudi skuli, pamoja na kuwashajihisha akinamama
kujikusanya na kuanzisha ushirika.
“Kweli hifadhi hii imekua nimkombozi mkubwa kwa wananchi wa kijiji cha
Sangaiwe na Vijiji jirani, wananchi walikuwa wakiona uhifadhi kama madhila sasa
wanajua umuhimu wake,’’anasema.
Mwenyekiti hifadhi ya jamii Burunge WMA Khamis Juma Mgimba, anasema
Sangaiwe ni moja ya vijiji ambavyo vinamuingiliano mkubwa na kimepakana na
hifadhi ya Tarangire.
Aidha kina wanyama wengi tafauti vijiji vyengine vilivyopakana na
hifadhi ya Burunge.
“Kwa sasa tupo na wataalamu kutoka chuo cha Nelson Mandela Arusha,
wataweza kuwaweka teknolojia ya kamera itakayo tusaidia katika vijiji, kubaini
wanyama wapi wamepita,”anasema.
JET
Chama cha waandishi wa habari za Mazingira Tanzania (JET), kupitia
mradi wa USAID “Tuhifadhi Maliasili” wakizungumza na timu ya wanachama wao, Mkurugenzi
mtendaji wake John Chikomo, amesema JET inatekeleza mradi wa miaka mitano.
Ambapo mradi huo wa Tuhufadhi Maliasili, ulianza na mafunzo na baadae
ni kutembelea katika shoroba sita zinazofanyiwa kazi.
Anasema kazi kubwa ni kuona waandishi wanazidi kuandika habari za
uhifadhi, wanyamapori na shoroba kwa uhakika, likiwemo kundi la wanawake.
MWISHO
Comments
Post a Comment