NA HASSAN MSELLEM, PEMBA
MAHKAMA ya Mkoa Chake Chake, imemuhukumu kutumikia Chuo Cha Mafunzo kwa muda wa miaka 14, mshitakiwa Omar Songoro Hamad mwenye miaka 38 mkaazi wa Vikunguni wilaya ya Chake chake, baada ya kupatikana na kosa la kumlawiti mtoto menye miaka 11.
Hukumu hiyo imetolewa jana Mei 18, mwaka 2022 na hakim Muumin Ali Juma wa mahakama ya maalum ya makosa udhalilishaji katika Mahakama ya mkoa Chake Chake.
Awali ilitajwa mahakamani hapo na Mwendesha mashtaka wa Serikali kutoka ofiai ya Mkurugenzi wa Mashtaka Mohamed Said Mohamed kuwa, mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo siku na tarehe isiyofahamika majira ya 1:30 usiku.
Ambapo alitenda kosa hilo, eneo la Vikunguni Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, akijua kuwa analofanya ni kosa.
Mashahidi wa nne wa upande wa mashtaka waliwasilishwa mahakamani hapo, akiwemo mtoto mwenyewe, mamzazi wa mtoto, Askari wa ,mpelelezi pamoja Daktari ambapo amekiri kuwa mtoto huyo alifanyiwa ulawiti.
Hakukuwa na mashahidi kwa upande wa mshitakiwa, na kumlazimu kujitetea mwenyewe, ambapo utetezi wake haukuweza kumnasua kwenye makucha ya hatia.
Kutokana na ushahidi uliotolewa na mashahidi wote wa nne, Mahakamani hapo ulimfanya Hakimu Muumin Ali Juma kumtia hatiani mshitakiwa Omar Songoro Hamad, na kumuamuru kutumikia chuo cha mafunzo kwa kipindi ch miaka 14 ili iwe fundisho kwake na kwa wengine wenye tabia chafu kama hiyo.
Mwisho.
Comments
Post a Comment