NA FATMA HAMAD, PEMBA
HAKIMU wa mahakama Mkoa Wete, Mwendesha
mashtaka, Karani, na askari wa mahakama, wamepigwa na butwaa baada ya baba
mzazi wa mtuhumiwa wa ulawiti, kudai mtoto wake ni kiziwi.
Awali
mtuhumiwa huyo alikuwa ni mzungumzaji mzuri, wakati kesi yake ikiendeshwa mahakamani hapo kabla ya kuondolewa kwa madai ya kudanganya
umri.
Ilibainika
kuwa wazazi wa kijana huyo mwenye miaka 19, anaedaiwa kumlawiti kijana mwenzake
mwenye ulemavu wa akili na kisha kupandishwa katika mahakama ya mkoa B Wete, Febuari 13, mwaka huu ingawa kesi yake
iliondolewa mwezi Machi mwaka huu baada ya kudaiwa kudanganya umri.
Ndipo
mahakama ya mkoa ‘B’ ilipompandisha kwenye kizimba chake na kusomewa upya
shtaka lake, kama mtu mzima, ingawa baba mzazi
kabla ya mtoto wake [mtuhumiwa] kujibu lolote, alidai kuwa ni kiziwi.
Hoja ya
mzazi huyo, ilichukua takriban dakika mbili mahakamani hapo, ikijadiliwa baina
ya hakimu, mwendesha mashtaka na baba mzazi, juu ya ulemavu ulioibuka ghafla na
kuwashangaaza waliokuwepo mahakamani hapo.
“Mheshimiwa
hakimu, mwanangu ni kiziwi ‘hawezi kuzungumza’, hivyo naomba nimsemee juu ya
kesi yake , pamoja na masuali yatakayoulizwa
mahakamani hapo,’’alidai baba mzazi.
Mwendesha
mashtaka, kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa mashataka Juma Ali Juma aliingilia kati
na kupinga vikali na kuiomba mahakama, isimtambue baba huyo kama wakala wa
mtuhumiwa na kutaka mtuhumiwa apelekwe Hospitali kwa ajili ya uchunguzi.
‘’Mheshimiwa hakimu kama mtuhumiwa leo hii ni kiziwa (anaulemavu wa matamshi)
basi taratibu zifuatwe kwa mujibu wa sheria, ikiwemo kupelekwa Hospitali kwa
ajili ya uchunguzi ili tuendelee na
shauri hili,’’ alidai mwendesha mashtaka.
Baada ya
mabishano hayo, hakimu wa mahakama ya mkoa ‘B’ Wete Ali AbdulI-rahman Ali alikubali na kulighairisha shauri hilo
hadi Mei 9, mwaka huu, ili kutoa nafasi kwa mtuhumiwa kupelekwa Hospitali kwa
ajili ya uchunguzi ili kubainika ikiwa ni kiziwi ama laa.
“Kama mtuhumiwa Kombo Nuhu Kombo ana ulemavu
wa matamshi, mahakama haina tatizo na hilo, na wale mashahidi kwanza musiwalete
mahakamani, mpaka apelekwe Hospitali na kupata maelezo ya mtaalamu,’alisema
Hakimu’.
Awali
mtuhumiwa huyo, alipandishwa mahakamani hapo akikabiliwa na tuhuma za kumlawiti
kijana mwenye ulemavu wa akili, mwenye miaka 19, jambo ambalo ni kosa kisheria.
Ilidaiwa mahakamani
hapo kuwa, kufanya hyivyo ni kinyume na kifungu cha 116 [1] cha sheria ya
Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018 sheria ya
Zanzibar.
Comments
Post a Comment