WASHIRIKI wa mafunzo juu ya namna
bora ya ujenzi wa amani na kujiepusha na migogoro hasa ya kisiasa ambao ni
wanaasasi za kiraia kisiwani Pemba, wamesema sasa wamepata uwelewa mkubwa wa
utatuzi wa migogoro hiyo.
Walisema,
elimu waliopewa kupitia mradi wa ‘Jenga amani yetu Zanzibar’ unaoendeshwa na ZLSC
kwa kushirikiana na tasisi ya Search for Common Ground na LHRC, imewapa mwanga
mkubwa.
Walisema,
awali walikuwa wakizijua mbinu za kienyeji za utatuzi wa migogoro na wakati
mwengine, walikuwa wakishindwa ingawa mafunzo hayo yamewajenga upya.
Hayo
waliyasema ukumbi wa mikutano Samail Gombani Chake chake Pemba, kwenye mafunzo yaliondaliwa
na ZLSC kupitia mradi wa jenga amani yetu.
Mmoja kati
ya washiriki hao Abrhaman Mbarouk Juma, alisema sasa amewiva vilivyo, kuweza
kuikinga au kuitatua migogoro ya kisasa itakapotokezea katika eneo lake.
Nae Is-haka
Sultan alisema, sasa wanaweza kuingia katika usuluhishi wa migogoro ya kisasa,
kwani elimu waliopewa kwa muda wa siku tatu, anajiamini.
“Tasisi hii
ya ZLSC, imekuja na mradi wa JENGA AMANI YATU Zanzibar kwa wakati, na mimi nimepata elimu ya
utatuzi wa migogoro ya kisiasa pamoja na mengine,’’alieleza.
Kwa upande
wake Maryam Said, alisema ingawa kwa migogoro mikubwa hana uwezo huo, lakini
kwa ile midogo midogo ya kisiasa anaweza kusaidia usuluhishi.
“Elimu ya
usuluhishi wa migogoro ya kisiasa ni muhimu mno kwetu, maana Zanzibar imekuwa
majeruhi wa kuingia katika migogoro inayotokana na siasa, kila baada ya miaka
mitano,’’alieleza.
Salama
Haroub alisema miongoni mwa mambo aliyojifunza kwenye mafunzo hayo, ni pamoja
na njia tano za kuitika mgogoro ikiwemo maelewano.
Njia
nyingine alisema ni kuvutana kwa lengo la kufikia suluhu, kushirikiana pamoja
na njia ya kusahameana kwa lengo la kuumaliza mgogoro husika.
Awali
akifungua mafunzo hayo Afisa Tathmini na ufuatiliaji kutoka ZLSC Khamis Haroun
Hamad, alisema mradi huo ni mahasusi kwa ajili ya kuijenga amani iliyopo.
Alieleza
kuwa, ni ukweli usiofichika kuwa, Zanzibar kila baada ya kumalizika kwa
harakati za uchaguzi mkuu wa vyama vingi, huwepo siuntafahamu miongoni mwa
wananchi.
Alieleza
kuwa, ili kuindeleza amani hiyo ambayo ni muhimu kwa mustakbali na ustawi wa
wazanzibari wote, ndio maana ZLSC, imeutafuta mradi huo maalum.
MWISHO
Comments
Post a Comment