NA HAJI NASSOR, PEMBA
KUTOKUWA na migogoro nchini ni sababu
kubwa inayopelekea kuendelea kwa shughuli za kimaendeleo na kufikia jamii yenye
amani.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Tathmini na ufuatiliaji wa mradi wa ‘Jenga Amani Yetu’,Khamis Haroun Hamad alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi juu ya nafasi ya wanasiasa kujenga amani ya Zanzibar.
Alisema, ili
jamii iweze kuwa na amani na kufikia
maendeleo endelevu, kunahitaji ushirikiano wa pamoja katika kutatuwa
migogoro inayoikabili jamii, huku wanasiasa wakiwa na nafasi kubwa .
Alifahamisha
kuwa, suala la kutatua migogoro si la mtu mmoja pekee, bali ni la watu wote, hivyo
ni vyema kila mmoja kuchukuwa nafasi yake katika jamii ili lengo liweze kufikiwa.
“Sisi
hatuwezi kutosha lakini tukichanganyika na nyinyi mukapeleka kwa wengine,
mafanikio yatapatikana kwa haraka”,alisema.
Alieleza
kuwa lengo la mradi huo ni kuifikia jamii na kuisambaza elimu hiyo, ili kila
mmoja ahakikishe analinda haki yake na ya mwenzake na kufikia heshima ya utu wa
mtu.
Kwa upande
wake Mratibu wa mradi wa jenga amani
yetu Zanzibar kutoka Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) Jamila Massoud,
alisema lengo la mradi huo ni kuibua changamoto za migogoro zinazojitokeza katika
jamii.
Alifahamisha
kuwa, makundi yote yanayopata mafunzo hayo yaendelee kuelimisha jamii katika kutatuwa migogoro, ili iweze
kuleta msaada katika maisha yao.
Katika hatua
nyengine, Jamila alisisitiza suala la ushirikiano kwa makundi yanayopatiwa
mafunzo hayo, ili kufikia maisha bora yenye maendeleo mazuri.
“Migogoro
mengi imeibuliwa, hapa sasa kunahitajika nguvu za pamoja, ili kuweza
kutatuliwa”,alisema.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Hafidh Abdi kutoka jumuiya ya KUKHAWA alisema migogoro iliopo kama haitoshughulikiwa vyema itapelekea kuongezeka kwa matatizo yasiyo ya lazima.
Nae mwandishi
Amina Massoud Jabir wa redio jamii Mkoani alisema ni vyema waandishi kuendeleza
kuandika habari za utatuzi wa migogoro ili jamii iweze kupata mafanikio.
Mradi wa
‘jenga amani yetu ‘ unatekelezwa mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Zanzibar
,kwa kushirikiana na kituo cha huduma za sheria Zanzibar na search for common ground
na LHRC kwa ufadhili wa umoja wa Ulaya.
Mwisho.
Comments
Post a Comment