NA HAJI NASSOR, PEMBA
WAANDISHI wa habari kisiwani Pemba,
wameshauriwa kuongeza bidii ya kuibua changamoto, zinazowakabili wananchi hasa
walioko vijijini, ili sauti zao ziwafikie wenye mamlaka kwalengo la kutatuliwa.
Hayo
yalielezwa na wanakongamano la kujadili uhuru wa kujieleza, uhuru wa habari na
maadili kwa waandishi wa habari, kwenye kongamano lililoandaliwa na Jumuiya ya
waandishi wa habari Pemba ‘PPC’ kupitia Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari
Tanzania ‘UTPC’ na kuwashirikisha waandishi wa habari wa Unguja na Pemba na
wadau lililofanyika Gombani Chake chake.
Walisema,
licha ya kazi kubwa inayofanywa na waandishi hao, lakini sasa waelekeze nguvu
zao zaidi vijijijini, ambako wananchi wanaoishi maeneo hayo, hawana msemaji wa
shida zao.
Mdau wa habari
Said Mohamed, alisema wananchi walioko vijijini wamekuwa na ukosefu wa taarifa
nyingi na kukosa baadhi ya huduma, hivyo waandishi wanayonafasi ya kuwasaidia.
Nae Msaidizi
Katibu wa Mufti Zanzibar, Sheikh Said Ahmad Mohamed, alisema katika kufanikisha
hilo, waandishi waendelee kujikita zaidi vijijini, ili kuwasaidia wananchi.
Mjumbe wa
Kamati tendaji ya PPC Dk. Amour Rashid, aliwashauri waandishi wa habri, kusoma
zaidi ya tasnia moja, ili waendane na kasi ya mabadiliko ya dunia.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii TV
Online Ali Massoud Kombo, alisema kama viongozi wataendelea kutumia nafasi zao
vibaya, kazi ya waandishi wa habari zinaweza kuwa nzito.
Akifungua
kongamano hilo, Msaidizi Mrajisi wa asasi za kiraia Pemba Ashrak Hamad Ali,
aliwataka waandishi kuendelea kuandika habari za maendeleo, ili kuwasaidia
wananchi.
“Kwa mfano,
kwa sasa kuna dhana ya uchumi wa buluu, ni wajibu wenu kuhakikisha
mnawaelimisha wananchi kwa kina, nini maana yake na faida kupitia vyombo
vyenu,’’alieleza.
Katika hatua
nyingine, Msaidizi huyo alisisitiza haja kwa waandishi kuendelea kutii bila ya
shuruti maadili yao, ili taifa kulibakisha salama.
Akiwasilisha
mada kwenye mafunzo hayo, Katibu mkuu wa ‘PPC’ Ali Mbarouk Omar, alisema moja
ya jukumu la mwandishi wa habari, ni kuelimisha na kukosoa.
“Kwenye
kukosoa, haina maana kuwa uandae migogoro baina ya waandishi na mamlaka husika,
bali iwe ni kukosoa kwa aili ya kujenga jamii,’’alieleza.
Msaidizi
Mwenyekiti wa PPC Khadija Kombo Khamis, aliipongeza UTPC kwa hatua ya kufanikisha
kongamano, hilo la kuelekea siku ya uhuru wa habari.
Mwisho
Comments
Post a Comment