HUDUMA ya kuzuia maambukizi ya virusi vya
Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ‘PMTCT’ ni huduma ambayo inawalenga
akinamama wajawazito na wenza wao.
Huduma hii ilianzishwa, baada ya kuona
kuwa asilimia 90 ya watoto chini ya miaka 15, wanaoishi na virusi vya Ukimwi inatokana
na maambukizo kutoka kwa mama zao na asilimia 10 iliyobakia, ndio ambayo
inatokana na sababu nyengine kama kusaidiwa damu na kubakwa.
Inakadiriwa vifo vya watoto chini ya miaka 15, vinavyotokana na virusi
vya Ukimwi katika dunia ni 610,000, ambapo kati ya hivyo vifo 550,000 vimetokea
katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania Zanzibar.
Maambukizi kutoka kwa
mama kwenda kwa mtoto, ni moja kati ya njia kuu zinazosababisha kuenea kwa kasi
ya maambukizi virusi vya Ukiwmi.
Maambukizi
hayo hutokea katika nyakati tofauti kama vile, wakati wa ujauzito, wakati wa
uchungu na kujifungua, wakati wa kipindi cha kunyonyesha maziwa ya mama.
Akinamama hao hasa wajawazito kwa asilimia
5 hadi 10 wamekuwa wakisababisha watoto wanaowazaa kupata maamimbizi.
Lakini inaonesha kuwa pia, asilimia 10
hadi 20 hutokea wakati wa uchungu na kujifungua jambo ambalo linahitajia
uangalizi wa kutosha.
Kwa upande mwengine asilimia 20 hutokea wakati wa mama mara baada ya
kujifungua anapomnyesha maziwa mtoto wake, ambao inawezekana alizaliwa akiwa
hana maambukizi kuyapata
Ndio maana wataalamu wanasema ikiwa kutakuwa na akinamama wajawazito 100, wanaoishi na virusi
vya Ukimwi wataachiwa wajifungue na kunyonyesha bila ya kinga, basi asilimia 40
tu, ndio watakaowaambukiza watoto wao virusi hivyo na watoto 60 watabaki wakiwa
salama na maambukizo hayo.
HUDUMA ZA
‘PMTCT’ NI NINI ?
Ni huduma inayotolewa kwa kila mjamzito kwa kupimwa maambukizi
ya virus vya Ukimwi kwa lengo la kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa
mtoto.
Mam mwenye maambukizi ya VVU anaweza kumuambukiza mtoto akiwa
tumboni, wakati wa kujifungua na wakati wa kunyonyesha.
Kwa mujibu ripoti ya Idara ya
Sera na Ushawishi ya Tanzania bara, inaeleza wastani ni akina mama wajawazito
wenye VVU 65 kati ya 100 wanapata huduma ya PMTCT.
Hata hivyo namba hiyo ni ndogo katika
mikoa ya Tanga, Rukwa, Mwanza, Morogoro, Mara, ambapo watoto hao wanapata
matibabu ya kuzuia wasiambukizwe na mama zao.
Ni wanne (4) tu kati ya 10 ikimaanisha kuwa sita (6) kati
ya 10 hawapati huduma za aina hiyo.
Ingawa ripoti imetaja sababu
kadhaa, zinazochangia hali hiyo ikiwa ni pamoja na, upungufu wa wafanya kazi wa
afya kwa ajili ya kutoa huduma za PMTCT na zile za matibabu kwa watoto.
Ripoti ikaeleza kuwa, leo hii
Tanzania kuna akina mama 118,000 wanaoishi na vvu kila mwaka, ambao wanawaambikiza
watoto wao karibu 40,000 kila mwaka.
Maambukizi haya ni sawa na watoto 118
wanaoambukizwa kila siku, na kama watoto hawa 40,000 wasipopata matibabu, nusu
yao watapoteza maisha kabla ya umri wa miaka miwili.
HUDUMA ZA ‘PMTCT’ ZILIANZISHWA LINI
?
Kwa Zanzibar huduma za kuzuia maambukizi ya virusi ukimwi kutoka kwa
mama kwenda kwa mtoto zimeanzishwa tokea mwezi wa Aprili 2005.
Ambapo kwa ushirikiano baina ya Wizara ya
Afya na mashirika ya maendeleo yakiwemo CDC, Columbia University, WHO, Medicos
del Mundo, UNICEF walifanikisha hilo.
HUDUMA
HIZI ZINA MALENGO GANI?
Kama ilivyo kwa huduma nyingine mbali
mbali, pia huduma hizi nazo zinamalengo kaadhaa moja wapo ni kupunguza
maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Aambapo njia hii hasa lengo lake ni kupunguza
maambukizo kwa watoto wachanga, ili kuona tunapata kizazi ambacho kiko huru na
virusi vya Ukimwi
Ambapo huduma hii inajumuisha mambo kadhaa
ikiwa ni pamoja na vipengele vya
huduma ya PMTCT, ushauri nasaha kuhusu maambukizi ya VVU kutoka kwa mama
kwamtoto.
Akizungumza na mwandishi wa makala hii, Kaimu
Mratibu wa Tume ya Ukimwi Pemba Ali Mbarouk Omar, alisema kipengele chengine
kinachojumuisha ni kuchunguzwa damu ya virusi vya Ukimwi.
Aidha alieleza kuwa,
jengine ni kutumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi, kuimarisha boresha huduma za uzazi.
“Huduma hizi zinaumuhimu mkubwa maana unaweza kumpa uhakika mama
mjamzito anaeishi na Virusi vya Ukimwi, kupata kizazi kilichosalama,’’anasema.
Mratibu wa kitengo shirikishi, kifua kikuu, homa ya ini ukomwa na
Ukimwi Pemba Khamis Hamad anasema wanasayansi wamefanikiwa kupata dawa za kuwasaidia
wagonjwa wa Ukimwi, ili kupungunza makali ya maambukizi (ARVs).
Anasema dawa hizi
zimechangia kupunguza maambukizo na vifo kwa kiasi fulani, ingawa inakadiriwa watu
14,000 huambukizwa VVU kwa siku.
Huku ikielezwa
kuwa, zaidi ya asilimia 95 ya maambukizo yanatokea kwenye nchi changa na zile
zenye pato la wastani.
Na jumla ya
maambukizo hayo hutokea kwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi miaka 49
wakiwemo wanawake kwa 50.
Anafafanua kuwa
asilimia nyingine 50 ni watu walio chini ya umri wa miaka kati ya 15 hadi 24.
Shirika la Afya
Ulimwenguni ‘WHO’ linaripoti kuwa jumla ya watu 8,500 hufariki dunia kila siku kutokana na ugonjwa wa Ukimwi.
Ambapo WHO linafafanua kuwa, zaidi ya asilimia 90
ya watu walioambukizwa wanaonekana katika nchi zinazoendelea, huku waengi wao
hawajijui kama tayari wameambukizwa.
Eneo
jengine Mraibu wa elimu ya mabadiliko ya tabia katika mradi wa afya kamilifu,
kutoka shirika la Amref help Afrika Sunday Beebwa, anasema vyombo vya habari vinamchango mkubwa wa
kuhakikisha kunazaliwa watoto wasio na maambikizi.
“Tayari tunaomama wajawazito katika familia zetu, namna ya wao kupata
watoto wasio na maambukizi tumekuwa tukifanyakazi kwa karibu na vyombo vya
habari ili kuelimisha hilo.
WAJIBU WA VIONGOZI
Kundi hili limetakiwa kushajiisha na
kuelimisha jamii kuhusu huduma ya kuzuia maambukizi ya virusi, katoka kwa mama
kwenda kwa mtoto.
Kaimu Meratibu wa Tume ya Ukiwmi Pemba Ali Mbarouk Omar, anasema ili
waelewe huduma hii ipo na umuhimu wake na hivyo waweze kuitumia.
Lakini akawataka wanaume na akinababa kuzitumia ipasavyo huduma hizi
kwani na wao zinawahusu kwa njia moja ama nyingine.
UKIMWI
Ukimwi
ni ugonjwa uliogunduliwa kwa mara ya kwanza huko nchini Marekani mwaka katika 1981,
huku mgonjwa wa mwanzo akionekana eneo
la Los Angeles nchini humo.
Ukimwi ulionekana barani
Afrika ya katika mwaka 1982, kuanzia hapo ugonjwa huo ulitapakaa katika nchi za
kusini, kaskazini, mashariki na magharibi ya Afrika.
Ingawa kusini mwa jangwa la Sahara hali ya Ukimwi
ilionekana kuwa mbaya sana ukilinganisha na sehemu nyengine duniani
UKIMWI KWA TANZANIA
Wagonjwa wa mwanzo waligunduliwa mkoa wa Kagera katika mwaka 1983,
ambapo miaka mitatu baadae, mikoa yote ya Tanzania ilikuwa tayari ina maambukizo
ya virusi vya Ukimwi.
Lakini kwa upande wa Zanzibar, wagonjwa watatu wa mwanzo wa Ukimwi
waligunduliwa katika 1986, eneo la hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja.
Maambukizo hayo ya Ukimwi yalienea sehemu mbalimbali ya visiwa hivi vya
Unguja na Pemba na tokea mwaka 1986 hadi mwaka 2015, idadi ya watu
walioambukizwa virusi vya Ukimwi imefikia 13,000.
Lakini asilimia 1 ya wamama wajawazito wameambukizwa na VVU, na
asilimia 86 ya maambukizi yako kati ya miaka 20-49, na watoto yatima zaidi ya
1500 wamerekodiwa kuwa wanaishi na maambukizi ya VVU.
Maraym Said Abdalla wa Chake chake
anaeishi na VVU kwa miaka 17 sasa, tayari ameshajifungua watoto wawili bila ya
VVU, baada ya kutumia njia elekezi za wataalamu wa afya.
Anasema, alikuwa karibu mno na wataalamu wa afya kila hatua ya kutafuta
na kuulea ujazito wake, hadi siku aliyojifungua.
‘Ninao watoto wawili ambao niliwapata nikiwa na Virusi vya Ukimwi,
lakini hasi sasa wako salama kama alivyo babayao,’’anabainisha.
Salim Ali Saleh ambae ni msimamizi wa mradi wa kuelimisha
jamii ya watu wanaoishi na VVU juu ya suala la lishe ya binadamu kutoka ZAPHA+
Pemba, anasema mama mjamzito na hasa mwenye VVU hutakiwa karibu na chakula
bora.
“Kama mama mjamzito ataacha kutumia chakula bora, mwilini
huathiri mfumo mzima wa chakula na kusababisha lishe duni ambayo hudhoofisha na
kuhatarisha afya yake,’’anasema.
Mwisho
Comments
Post a Comment