NA HAJI NASSOR, PEMBA::
MAHAKAMA
maalum ya makosa ya udhalilishaji mkoa wa kusini Pemba, asubuhi hii inatarajia kusikiliza utetezi wa mtuhumiwa Saymon Shija ‘mtuhumishi’ miaka (42) wa Machomane
Chake chake, anayedaiwa kumbaka mtoto wa miaka 4.
Mahakama hiyo chini ya
Hakimu wake Muumini Ali Juma, ilisema, hayo yanajiri baada ya wiki mbili
zilizopita, upande wa mashataka, kukamilisha na kufunga ushahidi wake.
Alisema, mashahidi wote
watano walioletwa mbele ya mahakama hiyo, na kisha kuongozwa na Wakili wa
serikali Ali Amour Makame, ulitosha kuonesha kuwa, mtuhumiwa huyo anahusika moja kwa moja.
Alisema, kwa ushahidi wa
awali, kwa kiasi ikubwa umeishawishi mahakama hiyo, kuamini kuwa mtuhumiwa
huyo, alimbaka mtoto wa miaka minne (4).
‘’Mshitakiwa, unanifahamu
kuwa, kwa ushahidi wa awali uliotolewa mahakamani hapa, na upande wa mashataka,
umekukuta na hatia, sasa unatakiwa ujipange ili uutie doa ushahidi
huu,’’alisema.
Hakimu huyo, alimfahamisha
mtuhumiwa huyo, njia tatu ambazo anaweza kuzitumia kwa ajili kufanya utetezi,
ikiwemo ya kiapo, bila ya kiapo na kukaa kimnya mahakamani hapo.
‘’Njia ya kukaa kimnya
upande wa mashataka hauwezi kukuliza suali, njia ya kiapo mahakama unauzingatia
na kisha utaulizwa maswali, ingawa bila ya kiapo hauzingatiwi sana na huulizwi,’’alimueleza Hakimu mtuhumiwa huyo.
Baada ya maelekezo hayo
kutoka kwa Hakimu, mtuhumiwa alichangua
njia ya kula kiapo, na kueleza kuwa, kwa siku leo Novemba 21, mwaka 2022 atakuwa tayari kujitetea kwa njia ya kiapo mahakamani hapo.
‘’Mimi nimechagua njia ya kujitetea kwa njia ya kiapo, na leo hii niko tayari samba mba na mashahidi wangu wawili, ambao watakuja kukana tuhma za kumbaka mtoto wa miaka 4,''alidai mtuhumiwa huyo.
Mwendesha mashataka wa serikali Ali Amour Makame, alidai kuwa hana pingamizi na uamuzi wa mahakama, na wa mtuhumiwa wa kujitetea kwa njia ya kiapo na kutumia mashahidi wake leo hii.
Hivyo Hakimu Muumini Ali
Juma wa mahakama hiyo, bada ya kushauriana na upande wa mashtaka, alilipangia
shauri hilo kurudi tena mahakamani leo Novemba
21, mwaka huu.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, mtuhumiwa
huyo Edson Syamon Shija ‘mtumishi’ (42), alidaiwa kumbaka mtoto
wa miaka minne (4), tukio lililotokea
Septemba 30, mwaka huu saa 2:00 usiku Machomane Chake chake.
Kufanya hivyo ni kinyume, na
kifungu 108 (1), (2) (e) na kifungu cha 109 (1) cha sheria ya Adhabu nambari 6
ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.
Mwisho
Comments
Post a Comment