NA
HAJI NASSOR, PEMBA:::
CHAMA
cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA-Zanzibar, kimewataka
wanamtandao wa kupinga matendo ya ukatili na udhalilishaji kisiwani Pemba,
wasikatishwe tamaa, kwa kuibuka kwa matendo hayo kila siku, ni ishara wananchi
wapeta uwelewa.
Hayo yameelezwa na Afisa Tathmini na ufuatiliaji kutoka TAMWA-Zanzibar
Mohamed Khatib, kwenye kikao cha siku moja cha kuwasilisha ripoti ya utendaji
kazi wa wanamtandao hao, kilichofanyika mjini Chake chake.
Alisema kazi kubwa imeshafanywa na inaendelea kufanywa na wanamtandao
hao, na ndio maana katika siku za hivi karibuni, wanaodhalilishwa wamekuwa
wakieleza.
Alieleza kuwa, ongezeko la takwimu ya matendo hayo pamoja na
wanaotendewa na hata watu wao wa karibu kuripoti, ni dalili kuwa, sasa jamii
imepata mwamko.
Afisa huyo aliwataka wanamtandao hao, kutokatishwa na tamaa na
ongezeko la matendo hayo, ambapo hilo linatokana na matumizi sahihi ya
kuifikisha elimu.
‘’Hivi sasa mtoto anadhalilishwa na baba yake, kaka yake, au mwalimu
wake na kisha anathubutu kutoa taarifa hizo, ni ishara kuwa, kila mmoja elimu
imemfikia,’’alieleza.
Hata hivyo, amewataka wanamtandao hao kisiwani Pemba, kuegemea zaidi
sasa katika mwaka ujao, kuishawishi jamii kufika mahakamani, kutoa ushahidi.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao hicho, Mratibu wa TAMWA Zanzibar
ofisi ya Pemba Fat-hya Mussa Said, aliwataka kuendelea na utoaji wa elimu kwa
jamii, ili kila mmoja atimize wajibu wake.
‘’Inawezekana baba anaona kama wajibu wa kumlea mtoto ni wa mama peke
yake, na yeye akishapata huduma za ndani, kama vile wajibu wake umekwisha,
jambo ambalo sio sahihi,’’alieleza.
Hata hivyo Mratibu huyo wa TAMWA, amepongeza kazi kubwa inayoendelea
kifanywa na wanamtandao hao, na hasa katika kuwafikia wananchi walioko
vijijini.
‘’Tutangalia namna ya kuwawezesha japo kidogo, ili mwaka ujao wa 2023,
muwe na uwezo wa hali na mali, kuwafikia wananchi wanaoishi katika visiwa
vidogo vidogo,’alileza.
Akizungumza katika kikao hicho, kwa niaba ya wanamtandao wa wilaya ya
Mkoani, Shaaban Ali alisema bado changamoto wanazopanga kuzifanyia kazi, ni
rushwa mauhali.
‘’Elimu tunatoa mno katika ngazi ya jamii, vyuo vya qur-an, skuli na
masokoni, lakini bado matukio mengine hayafiki mahakamanim kwa sababu ya
watendewa kutawaliwa na rushwa muhali,’’alieleza.
Nae Rashid Mshamata wilaya ya Wete, alisema matukio mengine ya ubakaji,
yanayowahusu watoto wenye miaka 16 na 17, ndio yanayoshindwa kuendelea, mbele
ya vyombo vya sheria.
‘’Anaweza kuja mzazi kwa hasira na kutaka mtuhumiwa aliyemdhalilisha
mtoto wake akamatwe hisia sasa na haraka, lakini kesi ikishafika mahakamani,
huanza kukosa ushirikiano, na kisha hufutwa,’’alieleza.
Mratibu wa wanawake na watoot shehia ya Kangagani Awena Salim Kombo,
alisema bado kesi zinazowahusu watoto wa viongozi, zimekuwa zikimalizwa kienyeji.
Nao mwanamtandao kutoka wilaya ya Wete Siti Faki Ali na mwenzake Haji
Shoka Khamis wilaya ya Mkoani, wameitaka TAMWA kwa mwaka ujao, kuangalia zaidi
elimu katika visiwa.
Akifungua kikao hicho Afisa mradi kutoka TAMW Zaina Salim Abdalla,
alisema kazi iliyopo mebele ya wanamtandao hao, sasa ni kuishawishi jamii,
kufika mahakamani kutoa ushahidi.
‘’Kwa ule Unguja, wananchi wameshahasika vyema, lakini kazi inakuwa
kwa wasimamizi wa sheria, na hasa kufuata haki kwenye eneo la
hukumu,’’alieleza.
Moja ya jukumu lake la msingi TAMWA ni kuhakikisha wanawake na watoto
wanaishi bila ya kukumbwa na majanga mbali mbali ikiwemo utelekezwaji,
udhalilishwaji na ukatili.
Mwisho
Comments
Post a Comment