NA HAJI NASSOR, PEMBA::
KIJANA Massoud Khamis Mussa wa
Vitongoji wilaya ya Chake chake, kuanzia Novemba 15 mwaka huu, ataendesha
maisha yake akiwa chuo cha mafunzo, kwa muda wa miaka 20, baada ya mahakama
maalum ya makosa ya udhalilishaji mkoa wa kusini Pemba, kumtia hatiani, kwa kosa la kumlawiti mtoto
wa miaka 9.
Mahakama
hiyo chini ya Hakimu wake Muumini Ali Juma, ilisema imefikia uamuzi huo, baada
ya mashahidi watano waliowasilishwa mahakamani kutoa ushahidi, ambao uilikidhi
vigezo husika.
Hakimu
Muumini alitumia dakika 35 kumsomea hukumu mshitakiwa huyo, ambapo alisema ushahidi
nambari moja ambao umetia hatiani mshitakiwa huyo, ni ule uliotolewa na mtoto
wa miaka 9.
Alisema mtoto
huyo, wakati anatoa ushahidi wake, aliithibitishia mahakama kuwa, mshitakiwa
Massoud Khamis Mussa, ndie mtu pekee ambae alishawahi kumlawiti akiwa bandani
kwake.
‘’Mtoto
alisema kuwa, siku ya kwanza kabla ya kulawitiwa, mshitakiwa alitumia mafuta ya
nazi, kuupaka uume wake na kisha nae kumpaka sehemu yake ya siri ya
nyuma,’’alisema Hakimu huyo.
Aidha Hakimu
Muumini alieleza kuwa, mtoto huyo alisema kwa siku ya kwanza, aliumia na kupiga
kelele ingawa hakuna aliyesikia na kutoa msaada, kwa vile banda hilo liko mbali
na makaazi ya watu.
Hata hivyo
Hakimu huyo, alisema shahidi mwengine aliyetoa ushahidi wake na kuipa nguvu
kesi hiyo ni daktari, ambae nae alithibitisha mtoto huyo kuingiliwa.
‘’Kikawaida
eneo la sehemu ya siri ya nyuma, imeumbwa kwa ajili ya kutoa kitu nje, ingawa
uchunguuzi wa kidaktari, uligundua tayari, kuna jambo limeingizwa na kutolewa,’’alifafanua
Hakimu kwenye maelezo ya huku yake.
Hivyo,
alisema ushahidi huo pamoja na wa askari mpelelezi, ulijitosheleza kuiaminisha
mahakama hiyo kuwa, mshtakiwa alimlawiti mtoto huyo.
Hakimu
Muumini alieleza kuwa, mtu pekee ambae anaweza kuithibitishia mahakama kuwa,
ameingiliwa ama kutoingiliwa ni muathirika na wengine wanaweza kujazia jazia.
Kabla ya
mshitakiwa huyo kusomewa hukumu yake ya miaka 20 kwenda chuo cha mafunzo na
fidia ya shilingi milioni 1, Mwendesha mashtaka wa serikali Ali Amour Makame, aliomba
mahakama hiyo, kutoa adhabu kali.
Alisema matendo hayo yamekua yakiathiri ndani
ya jamii, hivyo ni vyema, ikatolewa adhabu kali, ili wengine wenye tabia mbaya
kama ya mshitakiwa, waogope.
‘’Tayari
jamii ilishafanya wajibu wake, wa kuripoti kwenye vyombo vya sheria, na kisha
navyo kuchukua hatau za kuifikisha kesi hiyo, mahakamani hapa, sasa kazi
iliyobakia ni mahakama kutoa adhabu nzito,’’alisema Wakili huyo.
Awali
mshitakiwa huyo, alipopewa nafasi ya kuomba ahuweni, aliiomba mahakama hiyo,
kumpunguzia adhabu, maana anafamilia inayomtegemea.
Mshitakiwa
huyo ilithibitika kuwa, alimlawiti mtoto mwenye miaka 9, tukio lililotokea Septemba
14 mwaka huu, na kisha Septemba 22, lilkafikishwa mahakamani na kutolewa hukumu
Novemba 15, mwaka huu.
Ambapo hilo ni
kosa kinyume na kifungu cha 115 (1) cha sheria ya Adhabu nambari 6 ya mwaka
2018, sheria ya Zanzibar.
MWISHO.
Comments
Post a Comment