NA HAJI NASSOR, PEMBA:::
WANAFUNZI wenye mahitajia maalum
katika skuli mbali mbali kisiwani Pemba, wameikumbusha serikali kuzidi
kuimarisha miundo mbinu ya kielimu, ili watimize haki yao ya kupata elimu kwa ufanisi.
Walisema, bado serikali imekuwa
ikiweka mikakati zaidi kwenye maandishi, ingawa hawaoni utekelezaji wake hasa
kwa baadhi ya skuli, na kuendelea kuwaacha wao wakiwa kwenye mazingira magumu.
Wakizungumza na
mwandishi wa habari hizi kwa nyakati
tofauti, wasema wameshaitikia wito wa kwenda skuli kuungana na wenzao kutafuta
elimu, ingawa bado wamezungurukwa na cgangamoto.
Mmoja katia ya
wanafunzi Abdalla Hussein skuli ya Tumbe, alisema ukosefu wa vitabu vya nukta
nundu, waalimu wenye utaalamu ni moja ya changamoto zinazowakabili.
‘’Bado mazingira ya
sisi wenye mahitaji maalum katika skuli skuli zetu hayajakuwa rafiki kwa sisi
wenye ulembu wa aina mbali mbali, ni wakati wa serikali kuimarisha,’’alileza.
Nae mwanafunzi Asha
Hilali Hassan wa Mchanga mdogo, alisema uziwi alionao, imekuwa vigumu
kumfutilia mwalimu kuanzia mwanzo hadi mwisho.
‘’Unajua kwenye
mikakati na maandishi kuhusu siis kupatiwa elimu yako vizuri, ingawa kwenye
utekelezaji bado ni shughuli kubwa maana hatuoni manufaa,’’alifafanua.
Nae mwanafunzi asiyeona
wa skuli ya Mtambile Asha Ali na mwenzake wa skuli ya Kengeja mwenye ulemavu wa
usikivu, Mwanajuma Himid Maulid,wamesema bado mazingira yamekuwa dhaifu ya
kujifunzia.
‘’Zipo skuli
zinawaalimu wenye utaalamu wa kuwasomesha wenzetu wenye ulemavu, lakini ni
chache mno, sasa ni wakati kwa serikali kusambaaza vifaa visaidizi vya
kujifunzia,’’walisema.
Mzazi Asha Omar mwenye watoto wawili wenye
ulemavu wa viungo wa Konde wilaya ya Micheweni, alisema, bado idadi ya waalimu
wenye utaalamu wa kuwafundisha wanafunzi wenye mahitaji maaluma ni wachache.
‘’Tunakilio kikubwa
jamani watoto wetu wenye ulemavu hawasomi wanakaa tu majumbani na walioko skuli
kama vile wanawasindikiza wenzao,’’alilalamika.
Nae mzazi wa Salum Said Asaa mwenye mtoto asiyeona wilaya ya
Wete, alisema mtoto wake ameshindwa kuanza hata darasa moja, kwa kukosa huduma
ya nukta nundu.
‘’Mimi mtoto wangu alishafika darasa la pili, ila nimeshindwa
kumpeleka skuli kwani hakuna mwalimu wa kumfundisha yeye, bali namuacha aende
chekechea tu ili apoteze muda tu mana hata kwenye matokeo yake ni mabaya”,
alieleza.
Mjumbe kutoka Shirikisho
la Jumuia za watu wenye ulemavu Zanzibar ‘SHIJUWAZA’ Aziza Alawi Mussa alisema
licha ya changa moto hiyo ya uwepo wa uhaba wa walimu mjumuishi, aliwashauri
wazazi hao kuwapeleka skuli watoto wao.
‘’Kwanza niwanasihi
wazazi na walezi, ikifikia umri wa mtoto kwenda skuli, wafanye hivyo, ili hiyo
changamoto hiyo iwakute wakiwa katika mfumo wa elimu na sio nje,’’alieleza.
Mratibu
wa Baraza la taifa la watu wenye ulemavu Zanzibar kisiwani Pemba Mashavu Juma
Mabrouk, alisema suala la uhaba wa walimu mjumuishi ni tatizo, hivyo
ameishauri wizara ya elimu kuwapa kipaumbele
walimu ambao wamesomea fani hiyo.
Kaimu
Mratibu Elimu Mjumuisho na Stadi za Maisha ‘EMSM’ Pemba Halima Mohamed Khamis, alisema ujio wa dhana hiyo ndio
iliyokomboa watoto, wenye ulemavu na wale wenye mahitaji maalum, kupata haki
yao ya elimu.
Anasema,
awali watoto wenye ulemavu wa aina mbali mbali, waliachwa bila ya kupatiwa
elimu, kuanzia ngazi ya jamii na serikali kuu.
‘’Lakini
ilipofika mwaka 1991 serikali kupitia wizara ya Elimu ilianzisha madarasa
maalum, kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wa akili, ambapo kwa Pemba ni
skuli za Michakaini na Pandani msingi.
Kisha
mwaka 2006, sasa kukazaliwa dhana ya elimu mjumuisho, ambayo ni ule mpango wa
kuwaweka darasa moja kati ya wanafunzi wenye mahitaji na wale wa kawaida.
Anasema,
mpango huo ulianza kwa kusua sua, ingawa kwa wapo waalimu watano wenye Master,
10 wenye digrii, wakati wenye diploma 20 na 68 ngazi ya cheti wote wana fani ya
Elimu ya Mahitaji Maalum ‘SNE’
‘’Changamoto
hapa waalimu wanakimbia na wengine kubadilisha fani, maana hawapatiwi nyongeza
ya maslahi kwa kazi hiyo,’’alieleza.
Jumla ya
wanafunzi wenye uoni hafifu 803, wenye usikivu hafifu 690, wenye ulemavu wa
matamshi 405, wenye vichwa vikubwa na vidogo 22, umbikimo 13, mgongo wazi 7,
ulemavu wa akili 111, ulemavu mchanganyiko 113 na ulemavu wa viungo wanafunzi
91 wakiwa madarasani kutafuta elimu.
Mwisho
Comments
Post a Comment