Mhe. Pembe ameyasema hayo katika Maonesho ya mavazi ya wiki ya
ya Mafunzo ya Amali yanaliofanyika katika viwanja vya Mapinduzi Square
Michenzani Mjini Unguja, amesema mavazi ya staha ni moja ya Utamaduni wa wazanzibari
hivyo ni vyema kuendelezwa na kuacha kuiga mavazi ambayo hanastaha.
Amefahamisha kwamba mavazi
ya staha na malezi bora ni njia moja wapo ya kuzuia vitendo vya ukatili na dhalilishaji dhidi ya
wanawake na watoto ambavyo vinajitokeza kila mara ndani ya jamii.
“suala la kuiga tamaduni zisizo za kizanzibari ambazo baadhi
yake ndio sababu kubwa ya mporomoko wa maadili ya nchi na kusababisha vitendo
vya udhalilishaji kuongezeka kila siku ni vyema kuachana nazo na badala yake
kuendeleza mila, silka na Utamaduni wa Zanzibar” Alisema Waziri huyo.
Mhe. Riziki katika hafla hiyo ameomba Mamlaka ya Mafunzo ya
Amali pamoja na Vyuo vyengine kuanzisha madawati ya kijinsia katika vyuo vyao
ili iwe rahisi kwa wanafunzi wanapopata tatizo au kuona viashiria vya
Udhalilishaji waweze kutoa taarifa kwa haraka kuhusu kupinga vitendo vya
udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto.
Aidha ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao katika vyuo hivyo vya
Mafunzo ya Amali ili kupata taaluma na ujuzi utakaowasaidia vijana kupata ajira
na kujiongezea kipata hali ambayo itawasaidia kuinuka kiuchumi.
Mwisho amewaomba Wanafunzi waliomaliza mitihani yao ya Kidato
cha nne na hata wale ambao wapo majumbani kujiunga na vituo/vyuo vya mafunzo ya
amali kwani ni miongoni mwa fursa za kuweza kujiajiri na kuondokana na umasikini.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali
Zanzibar Dkt.Bakari Ali Silima amesema maonesho ya mavazi ni moja wapo ya
kuonesha kazi zinazofanywa na vyuo hivyo, hivyo ni vyema jamii kuangalia ili
kujifunza na kuona ni sehemu sahihi ya kuwapeleka watoto wao kupata ujuzi.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mavazi hayo Fatma Ali
amesema vazi la staha linasaidia kumpa
mtu ujasiri wa kukutana na watu mbali
mbali katika harakati za maisha kwani mavazi ni mawasiliano katika jamii
husika.
Comments
Post a Comment