MKUU wa mko wa kusini Pemba Mattar Zahor Massoud na Mkuu wa wilaya ya Chake chake Rashid Abdalla Ali, leo waliungana na baadhi ya viongozi wa chama, serikali, vikosi vya ulinzi na usalama na wananchi wingine pamoja na wafanyakazi wa serikali, katika usafi uliofanyika barabara ya uwanja wa ndege Pemba.
Ambapo zeozi hilo ni ishara ya uzinduzi wa shamra shamra za kuelekea miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, yalioasisiwa Januari 12, mwaka 1964.
Kisha Mkuu huyo wa Mkoa aliwahutubia wananchi na kuwataka wayalinde mapinduzi ya Zanzibar, kwani ndio yaliowakomboa wanyonge wa taifa hili.
Lakini akawakumbusha wannachi kuwa, ndani ya miaka hii 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, mkoa unao miradi ya maendeleo 23, ikiwemo miradi tisa ya uwekaji mawe ya msingi, miradi 10 itafunguliwa na miradi minne itazinduliwa ndani ya mkoa huo pekee.
Akaeleza kuwa, zoezi la kufanya mapainduzi ya Zanzibara hapo mwaka 1964, lilikuwa gumu na zito, ingawa waasisi wa taifa hili walifanikiwa na sasa kila mmoja ameshayaona matunda hayo.
Alifahamisha kuwa, inapotajwa Mapinduzi daima maana yake ni kuendeleza maendeleo mbele kwa ajili ya wananchi mbali mbali tena bila ya ubaguzi.
Mkuu wa wilaya ya Chake chake Rashid Abdalla Ali, alisisitiza kuendeleza utamaduni wa usafi kila siku na kila wakati
Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mattar Zahor Massoud, akikata majani kwenye zoezi maalum la usafi, kwenye barabara ya uwanja wa ndege Pemba, ikiwa ni uzinduzi wa shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar
Wapigaji wa vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na wale wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakimskiliza Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba, Mattar Zahor Massoud, mara baada ya kukamilika kwa zoezi la usafi kwenye barabara ya uwanja wa ndege Pemba, ikiwa ni uzinduzi wa shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar
Mkuu wa wilaya ya Chake chake Abdalla Rashid Ali, akikata majani, pembezoni mwa barabara ya uwanja wa ndege Pemba, kwenye uzinduzi wa shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar
wafanyakazi wa ZBC wakipamba nje ya jengo lao eneo la Mkajuni wilaya ya Chake chake, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, awali zoezi hilo lilitanguliwa na usafi katika jengo hilo
Comments
Post a Comment