Na Amina Mchezo, Zanzibar@@@@
Waandishi wa habari wanawake wananafasi na mchango mkubwa katika kuielimisha jamii kupitia mitandao ya kijamii kukizingatiwa usalama wao.
Akifungua mafunzo ya siku mbili Kwa waandishi wa habar wanawake Zanzibar mkufunzi na mwanahabar mkongwe kutoka nchini Kenya Cecilian Maundu amesema wanahabar wanawake wamekuwa wakipitia wakati mgumu wakiwasilisha kazi zao za kimtandao ukilinganisha na wanahabar wakiume.
Amesema hali hiyo huwawia vigumu baadhi ya waandishi kuendelea na kazi yao na wengine kuathirika kisaikolojia kutokana na baadhi ya wafuasi wa kimtandao kuwatolea maneno ya kashfa pasi na wao kuridhia.
Maundu amesema hali hiyo inaweza ikaondoka au kusaidiwa endapo kutakuwa na ushirikiano wa pamoja kati ya waandishi na taasisi za kihabar ili kuunda kikosi kazi ambacho kitamlinda mwandishi pale tu anapopata kadhia ya kimtandao.
"Zanzibar mnapaswa kutumia taasisi hizi kama ZPC, TAMWA, MCT na nyengine ili pale kuona mnashambulia Kwa pamoja mitandaoni kukomesha udhalilishaji huu." ameongeza Cecilian.
Hata hivyo amewatahadharisha wanahabar wanawake kuacha kuweka taarifa zao binafsi mitandaoni kwani baadhi ya wakati huwageukia na kutumika katika udhalilishaji.
"Kama mwanahabar anataka kuweka taarifa zake binafsi basi lazima azifiche na aweke neno la Siri (password) ambayo watu hawataweza kuingia la si hivyo taarifa hizo mwisho wake huwa mwiba kwake" Ameongeza
Wakitoa michango yao waandishi waliopatiwa mafunzo hayo Kwa niaba ya wengine Mwanahabar Najjat Omar kutoka The Chanzo online na Khairat Haji kutoka Chama Cha waandishi wa habar wanawake Tanzania TAMWA-ZANZIBAR wamesema hali ni mbaya Kwa waandishi wanawake pale wanapowasilisha kazi zao mitandaoni hasa pale wanapokosa msaada kutoka kwenye taasisi husika.
Mafunzo hayo ya siku mbili yaliobeba ujumbe wa Namna ya kuwa salama mtandaoni yamedhaminiwa na shirika la Pen America kutoka nchini Marekani.

mwisho
Comments
Post a Comment