NA HAJI NASSOR, PEMBA::::
MWALIMU
wa skuli ya Madungu msingi Ali Makame Khatib miaka 25, anayetuhumiwa kumbaka
mwanafunzi wake, amerejeshwa tena rumande na mahakama maalum ya makosa ya
udhalilishaji, baada ya upande wa mashtaka kutopokea shahidi mpelelezi.
Baada ya kufika mahakamani
hapo akitokea rumande, Mwendesha mashataka kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa
mashtaka Ali Amour Makame, alidai kuwa, shauri hilo lipo hatua ya kusikiliza
ushahidi.
Alidai kuwa, walitarajia kumpokea
shahidi ambaye ni Askari mpelelezi, ingawa hakutokeza mahakamani hapo, na wala
upande wao, hawana taarifa za dharura yake.
‘’Ni kweli mheshimiwa
hakimu, shauri hili la mwalimu wa skuli ya Madungu, tulitarajia kumsikiliza
shahidi wetu wa mwisho ambae ni askari mpelelezi, ingawa hakufika mahakamani
hapa,’’alidai.
Hivyo wakili huyo, aliiomba
mahkama hiyo, kuliahirisha shauri hilo na kulipangia siku nyingine, ili
kuendelea na utaratibu mwengine mahkamani hapo.
Baada ya maelezo hayo, Hakimu
wa mahkama hiyo maalum ya makosa ya udhalilishaji, Muumini Ali Juma, alikubaliana
na ombi la upande wa mashtaka, na kuliahirisha shauri hilo hadi Oktoba 11,
mwaka huu.
‘’Wakili wa upande wa
utetezi una hoja yoyote, baada ya maelezo ya wakili wa upande wa mashataka, na
kama huna basi mtuhumiwa arudi tena rumande, hadi siku hiyo na shahidi
aliyebakia aitwe,’’alisema Hakimu.
Wakili wa upande wa utetezi
Suleiman Omar, alikubaliana na ushauri wa upande wa mashataka, na kuiomba
mahakama hiyo kulipanga shauri hilo tarehe fupi.
Awali ilidaiwa mahakamani
hapo kuwa, mtuhumiwa huyo Ali Makame Khatib, mkaazi wa Matuleni wilaya ya Chake
chake, alidaiwa kumbaka mtoto wa miaka 11.
Aambapo kufanya hivyo ni
kinyume na kifungu 108 (1), (2) (e) na kifungu cha 109 (1) cha sheria ya Adhabu
nambari 6 ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.
Tuhma ya pili alilitenda
August 12, mwaka huu majira ya saa 11:30 akiwa skuli ya Msingi Madungu wilaya
ya Chake chake, ambapo alidaiwa kumbaka mtoto huyo.
Mwisho
Comments
Post a Comment