Skip to main content

MIRADI YA MAJI KUKABIDHIWA DISEMBA 2022

 


Na Salma Lusangi:::::

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Maji Nishati na Madini Mwanajuma Majid Abdullah amesema Wizara yake inatarajia kukabidhiwa miradi ya maji ifikapo Disemba mwaka huu, hivyo amewaomba wananchi wawe na subra kwani miradi hiyo imefikia asilimia 80 ya utekelezaji wake ikiwemo wa uchimbaji wa visima, ulazaji wa mabomba na ujenzi wa Matangi ya maji.

Akizungumza mara baada ya kushiriki ziara ya pamoja na kamati ya Ardhi, Mawasiliano na Nishati ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika maeneo mbali mbali ya miradi hiyo. Alisema anafahumu kwamba tatizo la maji halistahamiliki lakini amewaomba wananchi kuendelea kupokea huduma ya maji kwa mgao kwani sio muda mrefu tatizo la maji litamalizika Zanzibar.

Alisema tatizo la maji Zanzibar limetokana na uwepo wa visima vichache ambavyo vinatumika pamoja na uchakavu wa miondombinu ya maji lakini kupitia jitihada za Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi za kuwaondolea shida ya maji wananchi wake. Wizara ya Maji inaendelea kusimamia ipasavyo miradi hiyo ambapo ifikapo Januari, 2023 maji yatapatikana katika maeneo mengi ya Unguja na Pemba.

“Tumepiga hatua, tunamshukuru Mhe. Rais wa Zanzibar Dkt Mwinyi, miradi ya maji inayotekelezwa kwa fedha za Uviko 19, na fedha za Exim Bank ya India itakabidhiwa kwa Serikali Desemba, nimejionea mwenyewe ZAWA imefanya kazi kubwa, hivyo tatizo la uhaba wa maji litatatuka muda sio mrefu, naomba wananchi wamuunge mkono Mhe Rais kwa kustahamili kidogo tu” Alisema. Mwanajuma”

Naye Mkurugenzi Idara ya Huduma za Maji Mudrik Fadhil Abas alisema  kukamilika kwa miradi hiyo kusaidia maeneo mbali mbali ya wananchi kupata maji kwasababu matangi ya maji yaliyojengwa hayapungui 300 kwa Unguja na  Pemba hivyo asilimia kubwa ya wananchi watapata maji. Pia alisema na kila tangi limeshapangiwa maeneo ya kupeleka maji.

Alifahamisha kwamba mabomba ya maji yaliyolazawa kutoka kwenye kila tangi yanaupana wa nchi 12 hali ambayo itasaidia kufikisha maji kwa haraka katika maeneo yaliyokusudiwa ili wananchi waweze kuendelea na shughuli zao za kiuchumi na kijamii na kusahau kabisa tatizo la maji Zanzibar.





Kwa upande wake Kaimu wa kamati ya Ardhi, Mawasiliano na Nishati ya Baraza la wawakilishi Zanzibar Kombo Mwinyi alisema ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maji, lakini amesisitiza kwamba miradi hiyo imalizwe kwa wakati  unaotakiwa. Pia aliiagiza Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kuhakikisha kwamba wanawataalam wa wakutosha kwaajili ya kuendeleza usimamizi wa miradi hiyo.

Aidha alihoji changamoto ambazo zinaikabili (ZAWA) katika utekelezaji wa miradi hiyo kwa sababu hawapendi kusikia ifikikapo Mwezi Desemba miradi hiyo kuwa haijakamilika, kwani wananchi wamekabiliwa na tatizo la maji katika maeneo mengi ya Zanzibar.

Kwa Upande wake Mkurugunzi Mkuu ZAWA Mhandisi Dkt Salha Mohammed Kasim alisema changamoto ambazo zinamkabili ni uchelewaji wa vifaa kuingia nchini lakini changamoto kubwa inayomsumbua sana ni ukosefu wa wataalamu hivyo ameiomba Serikali kuzingatia na kulifanyia kwani hata miradi ikikabidhiwa  bado ZAWA inahitaji wataalamu kwasabau miradi inahitaji usimamizi wa hali ya juu.

Mwisho Mhandisi Dkt Salha aliihakikishie kamati hiyo kwamba ifikikao Desemba mwaka huu miradi ya maji itakabidhiwa, kutokana na hatua iliyofikiwa na juhudi zinazochukuliwa na taasisi yake.

Miradi ya Maji Zanzibar ikiwemo ujenzi wa matangi, ulazaji wa mabomba ,uchimbaji wa visima inatekelezwa kwa fedha za ahuweni Uviko 19 na fedha za Exim Bank ya India na itawanufaisha wananchi wote wa Zanzibar.

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 mchan

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’’ali

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa ufafan

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kutafuta matibabu nje ya nch