NA HAJI
NASSOR, PEMBA
WANANCHI kisiwani Pemba, wameshauriwa
kujiungu na vikundi vya mazoezi ya viungo, kwani vimejiwekea utaratibu mzuri,
ambao unapingana na utovu wa nidhamu kwa wanamaoezi.
Kauli
hiyo imetolewa na Katibu wa muda wa Umoja wa vilabu vya mazoezi ya viungo Pemba
‘PAFIC’ Khalfan Amour Mohamed, wakati akizungumza kwenye mafunzo ya siku moja,
kwa wanamazoezi wa vilabu hivyo, yaliyofanyika skuli ya msingi Mchanga mdogo wilaya
ya Wete.
Alisema,
wamekuwa wakisemwa vibaya na baadhi ya watu, kuwa ndani ya vilabu vya mazoezi
kuna kuvunjiana heshima, jambo ambalo sio sahihi.
Alieleza
kuwa, wamekuwa na utaratibu mzuri ambao jinsia moja na nyingine, hazivunjiani
heshima, hivyo kama wapo waliokuwa wakilihofia hilo, wasiwe na wasi wasi nalo.
Katibu
huyo wa muda alifafanua kuwa, wanachama wa vilabu vyote, wamekuwa wakielimishwa
kila siku, juu ya umuhimu wa kuheshimiana na kulindiana nidhamu, ili lengo la
kufanya kwao mazoei lifikiwe.
‘‘Kama
wapo wananchi wenzetu walikuwa na wasiwa wasi, na vilabu vya mazoezi kwamba
vina jambo jengine lililokinyume na maadili linafanyika, waondoe shaka hiyo na
vikundi viko salama,’’alieleza.
Akizufungua
mafunzo hayo Afisa Mdhamini wizara ya habari, vijana, utamaduni na Michezo
Pemba, Mfamau Lali Mfamau, alivishauri vilabu vya mazoezi, kuanzisha na michezo
mengine ndani yake.
Alieleza
kuwa, kwa vile lengo lao ni kufanya mazoezi kama afya, sio vibaya wakaangalia
kushiriki kwenye michezo kama mpira wa miguu, mikono, kikapu na mpira wa meza
ili kuongeza idadi ya wanachama.
‘‘Inawezekana
hamupati watu wengine kwa sababu, wengine hawapendi kufanya mazoezi ya viungo
pekee, lakini kama mtaanzisha michezo mengine itakuwa sehemu pia ya
kuifufua,’’alieleza.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa muda wa Umoja wa vilabu vya mazoezi Pemba Ali Hamad,
alisema mafunzo hayo ni kwa ajili ya waalimu wa mazoezi na wasaidizi wao,
ingawa hapo baadae itakuwa ni kwa ajili ya wanachama wengine.
Alisema,
mafunzo hayo yalitokana na vikao mbali mbali ya viongozi wa vilabu vya mazoezi
kutoka wilaya nne za Pemba, baada ya kuwepo changamoto ya nidhamu kwenye vilabu
vyao.
‘’Ndio
maana ili kujiweka sawa kama tasisi, tumewafundisha nani mwalimu bora, nini
maana ya mazoezi, mbinu za kufundisha mazoezi na kuchunga nidhamu,’’alieleza.
Mkunzi wa
mafunzo hayo, Mwalimu Talib Ali Rajab, alisema kati ya sifa kadhaa za mwalimu
bora, miongoni mwao ni kujiheshimu, nidhamu, kujiamini na kujenga upendo.
‘’Lakini
pia mwalimu anatakiwa awe mbunifu, anayependa kujitolea, kuwajali wenzake,
kuwaunganisha, kujiepusha na migogoro pamoja na kuacha vitendo vya
udhalilishaji,’’alieleza.
Kwa
upande wake mkufunzi Ali Siyahi, alisema mwalimu wa mazoezi anatakiwa ajiepushe
na kufanya vitendo kwa kasi, kwani wapo baadhi ya wazee hawahimili hilo.
Wakichangia
mada kwenye mafunzo hayo, mwanamazoezi kutoka Gombani Fitness Club Ali Mbarouk
Omar, alisema suala la uvumilivu kwa mwalimu ni sifa nzuri kujipambana nayo.
Nao Kassim
Ahmed Seif na Siti Hamad Massoud, walisema kwa vile lengo ni kuwa na afya bora,
hakuna haja ya kufanywa vitendo vya kiungo kwa haraka kupitilia.
Mafunzo
hayo yalioandaliwa na Umoja wa Vilabu vya mazoezi ya viungo Pemba ‘PAFIC’ yalivishirikisha
vilabu vya Gombani Fitness Club, KMKM Wete, Gando, New Solution, Shumba,
Kisauni, Tumbe, Zaphias Chake chake na Mkoani pamoja na wenyeji Kambini Fitness
Club.
mwisho
Comments
Post a Comment