NA
HAJI NASSOR, PEMBA:::
MAHKAMA
maalum ya makosa ya udhalilishaji mkoa kusini
iliyopo Chake chake, imelazimika kumrejesha tena rumande mtuhumiwa
Khamis Haji Chumu ‘soda’ miaka 76, anayekabiliwa na makosa mawili, likiwemo la
ubakaji, baada ya ombi lake la dhamana, kutosikilizwa na mahakama kuu.
Awali mtuhumiwa huyo akiwa
na wakili wake, wameshapeleka ombi la dhamana yake mahakama kuu wiki iliyopita,
hivyo kwa vile mahkama hiyo, bado halijalikalia kitako ombi hilo, amelazimika
kurejeshwa tena rumade.
Mara baada ya kuwasili
mahkamani hapo akitokea rumande, mtuhmiwa huyo, bila ya kuwepo kwa wakili wake,
alidai kuwa hana taarifa zozote, ikiwa ombi lake limeshasikilizwa ama laa.
Hakimu wa mahakama hiyo
Muumini Ali Juma, alimuuliza mtuhumiwa huyo, ikiwa ameshaarifiwa na wakili wake
juu ya kupatiwa au kukataliwa kwa dhamana, na kujibu hana taarifa rasmi.
‘’Mtuhumiwa wewe na wakili
wako mlipeleka ombi la dhamana mhakama kuu, kutokana na hali yako, jee mmefikia
wapi, na leo (jana) hata wakili wako hayupo mahakamani,’’alihoji Hakimu
Muumini.
Mthumiwa huyo, alidai
mahakamani hapo kuwa, hana taarifa za wapi wakili wake alipo, wala suala la
kuwa ombi lake limeshasikilizwa ama laa na mahkama kuu.
Awali Mwendesha mashtaka
mahakamani kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Ali Amour Makame alidai
kuwa, kwa sasa shauri hilo, limesimama mahakamani hapo, hadi hapo mahkama kuu,
itakapotoa uamuzi wa dhamana.
‘’Ni kweli mtuhumiwa
anakabiliwa na makosa mawili, moja la kutorosha na la pili kubaka, lakini
alishatuma ombi la dhamana mahakama kuu, lakini bado halijasikilizwa,’’alidai.
Hivyo baada ya maelekezo
hayo, hakimu Muumini aliamuru mtuhumiwa huyo, kurejesha tena rumande na kurudi
tena mahakamani hapo Oktoba 10, mwaka huu wakati mahakama kuu, ikitarajiwa
kusikiliza ombi lake Oktoba 19 mwaka huu.
Awali ilidaiwa mahakamani
hapo kuwa, mtuhumiwa huyo Khamis Juma Chumu ‘soda’ (76) mkaazi wa Mtoni
wilaya ya Chake chake, alidaiwa kumtorosha mtoto wa kike miaka 13, wakati
akienda kuchota maji mferejini na kumpekea nyumbani kwake.
Kufanya hivyo ni kosa,
kinyume na kifungu 113 (1) (a) cha sheria ya Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018, sheria ya
Zanzibar.
Kosa la pili ni la ubakaji, ambalo
anadaiwa kulifanya Mei 15, mwaka huu, ambapo anadaiwa kumbaka mtoto mwenye
miaka 13 majira ya saa 4:15 asubuhi, eneo la Mtoni wilaya ya Chake chake.
Ambapo kufanya hivyo ni
kinyume, na kifungu 108 (1), (2) (e) na kifungu cha 109 (1) cha sheria ya
Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.
Mwisho
Comments
Post a Comment