NA
HAJI NASSOR, PEMBA
MTUHUMIWA
wa ubakaji, Sabour Juma miaka 47 mkaazi wa Chanjaani wilaya ya Chake chake,
ameiambia mahkama ya makosa ya udhalilishaji ya mkoa wa kusini Pemba
iliyopo Chake chake kuwa, muda aliyodaiwa kuwa amebaka, alikuwa kwake akipiga
msuwaki.
Alidai kuwa, maelezo ya
mashahidi kuwa majira ya asubuhi alimuingiza mtoto wa miaka 11 ndani ya choo
cha nyumbani yake sio sahihi, kwani muda huo alikuwa nje ya nyumba akipiga
msuwaki ‘akisugua meno’.
Aliyadai hayo mbele ya
mahakama hiyo, chini ya Hakimu Muumini Juma Ali, wakati mtuhumiwa huyo
aliyekuwa akiongozwa na wakili wake Suleiman Omar, akijitetea, baada ya upande
wa mashtaka kufunga ushahidi wao.
Alidai kuwa, familia ya
mtoto huyo inachoyo naye na imemtengenezea mazingira ili kumshitaki na
kumfungisha, na wala hakumumbuki kumbaka mtoto huyo.
‘’Sikumbuki kumbaka mtoto huyo
wa miaka 11, aliyekuja kutoa ushahidi mahakamani hapa, bali wamenitengenezea
zengwe kwa njia ya kunibambikizia kesi hii,’’alidai.
Aidha mtuhumiwa huyo, alidai
kuwa hana mazoea na mtoto huyo, na wala hawajahi kumpa fedha za matumizi ya
skuli, kama alivyodai, wakati akitoa ushahidi wake.
‘’Hata kwangu hakuwa na
kawaida ya kuja, na mimi sikuwa nikimfahamu, bali siku moja moja humuona aidha
anakwenda au anarudi skuli,’’alidai.
Alipoulizwa na wakili wake,
Suleiman Omar Suleiman kwa vile ameshamuacha mke wake kwa zaidi ya miaka mitatu
sasa, anafanya nini anapojiskia kutaka kufanya tendo la ndoa, na alidai hafanyi
maana ni kosa kwa Muumba.
‘’Ni kweli mke wangu nimeshamuacha kwa miaka mingi, lakini mimi hata nikijiskia kutakufanya tendo hilo, hujikataza maana kisheria ni kosa,’alisisitiza mtuhumiwa huyo.
Baada ya mtuhumiwa pamoja na
wakili wake kumaliza kutoa ushahidi wao, Hakimu wa mahkama hiyo Muumini Ali Juma,
aliupa nafasi upande wa mashtaka, uliokuwa ukiongozwa na wakili Mussa Khamis
Ali na Ali Amour Makame, kumuuliza mtuhumiwa.
‘’Je mtuhumiwa Sabour Juma, utakubaliana
na mimi kuwa anayejua kuwa tendo la ndoa limefanyika ama halikufanyika ni kati
ya mwanake au mwanamme,’’aliiuliza wakili wa serikali Ali Amour.
Ambapo wakili huyo,
alimueleza mtuhumiwa kuwa, mtoto aliyembakwa alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ndie
aliyemfanyia vitendo vya ubakaji wakiwa chooni.
Wakili wa serikali nambari
mbili, Mussa Khamis Ali, alitaka kujua kutoka kwa mtuhumiwa huyo, sababu ya
yeye kuwepo mahakamani hapo.
Baada ya maswali ya mawakili
hao, Hakimu wa mahkama hiyo Muumini Ali Juma, aliupa nafasi upande wa utetezi
pamoja na mtuhumiwa wake, kujadiliana ikiwa wanaweza kuleta shahidi wa utetezi.
‘’Mheshimiwa baada ya
kuzungumza na mteja wangu, tumeona tupangiwe siku nyingine kuja kuendelea na
utetezi wetu, tukiwa na shahidi wetu siku hiyo,’’aliomba wakili wa utetezi.
Hakimu wa mahaka hiyo,
alikubaliana na ombi la wakili wa utetezi, na kuliahirisha shauri hilo hadi
Oktoba 11, mwaka huu.
Mapema Septemba 19, mwaka
huu mahakama hiyo ilimfutia kosa la utoroshaji mtuhumiwa huyo, na kuendelea na
tuhma moja ya ubakaji.
Ambapo tendo hilo anadaiwa kulifanya
Machi 10, mwaka huu kwa kumbaka mtoto wa miaka 11, ni kosa kinyume na vifungu vya
108 (1), (2), (e) na 109 (1) sheria ya Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018.
Mwisho
Comments
Post a Comment