Skip to main content

-MKUNGA, MWANAMKE KIONGOZI ALIYEANZA MBALI, AVIRUKA VIGINGI, 2030 KURUDI TENA JIMBONI

 


NA MARYAM SALUM, PEMBA@@@@

‘……kidogo kidogo ndio mwendo……’.

Ni msemo wa kiswahili unao maanisha kufanya mambo hatua kwa hatua, subira na umakini  ndiyo njia bora na salama ya kufanikisha malengo.

Msemo huu unaenda sambamba na safari ya Mkunga kutoka kazi ya Ualimu, hadi   ulingo wa kisiasa kuwa Makamo Mwenyekiti ngome ya Wanawake Taifa wa ACT.

                   TUMJUE MKUNGA.

Mkunga Hamad Sadala (65) ni mwanandoa, mchakarikaji, mwenye kujiami asiyekubali kuyumbishwa kwani anajitambua na anajikubali popote.

Alizaliwa mwaka 1961 katika Kijiji cha Uvumbi shehia ya Chanjaani Chake Chake, ni mtoto wa tano (5) na wa mwisho katika familia ya mzee Hamad Sadala.

Anasema kuwa mnamo mwaka 1966 hadi 1967  wazazi wake walimsomesha elimu  ya awali darasa la kwanza skuli ya Shamiani hadi mwaka 1978 kumaliza kidato cha tatu skulini hapo.

Anafahamisha kuwa mwaka 1979 aliendelea na  elimu yake ya kidato cha nne katika skuli ya Fidel Castro, na baada ya kumaliza tu darasa lake la kumi na mbili, aliajiriwa kuwa mwalimu mwaka 1980.

“Kumaliza tu elimu yangu ya Kidato cha nne, sikukaa niliajiriwa rasmi ualimu, kipindi hicho kazi inamtafuta mtu na sio mtu kutafuta kazi,” anaeleza.

Alifanya kazi yake ya kusomesha kutoka mwaka huo katika skuli mbalimbali, ikiwemo Mwanakwerekwe C, Michakaeni, Vitongoji, Wawi, na Mdungu.

Mwaka 2018, alistaafu kwa hiari katika skuli ya Vitongoji, na sasa amejikita zaidi kwenye masuala ya siasa, katika nafasi mbali mbali za kichama.

Kwa sasa ni mwanasiasa, hasa tokaa alipostaafu kazi yake, na ni mwanachama halali wa Chama cha ACT Wazalendo, na amekuwa kiongozi kwenye ngazi ya tawi, Jimbo,Mkoa na Taifa.

Anasema   sasa kwenye chama ni Makamo Mwenyekiti wa gome ya Wanawake Taifa, pia ni mjumbe wa halmashauri kuu Taifa kupitia Chama chake hicho.

Mkunga anaelezea nafasi mbali mbali ambazo aligombea kama mwanamke, tokea mwaka 2020 amesimama kidete kugombea nafasi ya Ubunge kwa bahati mbaya hakupita.

Mwaka 2025 anasema hakukata tamaa bali alijitokeza kugombea nafasi ya Ubunge Viti maalumu pia hakufanikiwa.



 “Sababu zakutofanikiwa zipo nyingi, ambazo hata yeye hakuwa tayari kuzitaja, ingawa wanawake wenzake walikwa wanamkubali,”anaeleza.

Anafahamisha kwenye siasa kumekuwa na changamoto nyingi, ikiwemo kuitwa majina mabaya kutukanwa, hivyo ustahamilivu ndio msingi wake mkuu.

Aneleza licha ya changamoto anazopitia katika kusaka uongozi Jimboni, bado anaendelea kuwa na subira, akiamini ipo siku itatiki tu, kwani kama ipo ipo tu.

Kwa upande wa Wanawake wenzake ushirikiano ulikuwa mkubwa na ulimpa matumaini yakufanikiwa Jimboni, lakini kutokana na sababu zisizoepukika zilimfanya yeye kutofanikiwa.

Anafahamisha kuwa upande wa kijamii anaishi vizuri, kwani anapokwenda sana kushauriwa na kila mtu na huo ndio utu na ili kufika mbali kunahitajika hayo.

“Katika jamii iliyonizunguka nathubutu kusema inanipenda sana, kwasababu hata mimi nawapenda iwe mkubwa, mdogo na hata awe chama chingine.

Anaeleza mtu yoyote anapoamua kuingia kwenye siasa ni vyema kuangalia ubinadamu kwanza, kwani kabla ulikuwa unaishi na jamii na utahitaji kurudi kwa watu baadae.

Kumbe anaona wala siasa si chaka la ubaguzi, fitna bali ni njia ya kujichanganya na watu zaidi na kukufanya kujulikana ndani, nje na hata kwenye mataifa ya mbali.

Anaeleza mwanamke kama kiongozi kwenye chama chake, atahakikisha anaendelea kuishi na jamii kwa mashirikiano, kwa hali na mali bila kujali nafasi yake, ili aweze kufikia malengo yake.

Mkunga, kukata tamaa kwake ni mwiko kwani moja ya ndoto zake ni kuwa kiongozi wakuchaguliwa na wananchi kwenye Jimbo lake, ili aweze kusaidia jamii katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

Nje ya siasa, Mkunga ni mwanaharakati wa elimu, na ndio maana aliwahi kumsaidia kijana ambae aliacha masomo, baada yakufanya mitihani yake ya darasa la saba kutokana na hali ya maisha yao kuwa duni.

 “Kama mwanamke mwenye nafasi kwenye Chama changu, sikuwa tayari kuona maisha ya kijana huyo yanafifia, nilihakikisha napambana, ili kumsaidia kijana huyo, aweze kurudi masomoni,’’anasema.

Kwa vile Mkunga ni mpenda maendeleo, hupenda kujishusha kwenye jamii na mwenye kuthamini taifa akiamui kuwa, vijana na wanawake ndio nguvu ya nchi pahala popote pale.

Eneo jingine, ilikutana na kijana huyo Ali Faki Mohamed, hamsahau Mkunga, akisema anamfananisha na mzazi, wake baada ya kumpania hadi kufikia kidato cha pili mwaka huu.

Ndio maana Mkunga anawashauri viongozi wengine wanaposhuhudia changamoto kama hizo, wala wasisubiri kila kitu serikali, wachukue hatua maana ndio uzalendo unaoimbwa kila siku.

 Baba mzazi wa kijana huyo Faki Mohamed Faki, anasema kuwa Mkunga anajua maana ya maendeleo, na ndio maana baada ya kusikia changamoto yam toto wangu, alichukua juhudi za haraka.

Anasema amekuwa akijitoa kwenye jamii yake, na kuhakikisha vijana wanasoma na kufikia ndoto zao, tena bila ya kujali chama wala aina ya familia.

“Mtoto wangu kama sio mwalimu Mkunga na uwanaharakati wake, basi angali potoka kwani alikuwa tayari kashajiingiza kwenye vikundi viovu, leo nashukuru yulo darasani,’’anasema.

Asha Hamad Khamis mkaazi wa Vitongoji anasema mwanasiasa huyo na kiongozi ni mtu wa watu, anapenda watu, anapendwa na jamii, yupo bega kwa bega, popote kwenye shughuli za kimaendeleo yuko mbele.

“Kwakweli simalizi kumuelezea kutokana na mambo mengi anayotusaidia iwe harusi iwe msiba, harakati za elimu na hata kupigia miradi ya maendeleo,’’anasimulia.

Mwanachama wa ACT Wazalendo Vitongoji Hadia Juma Faki, anasema Mkunga amekuwa mfano kwa wanawake wote wa ndani ya chama na wale wingine wa nje.

“Nikimzungumzia siasa yupo vizuri, anajiamini, anapenda ushauri, anajishusha, anapenda kushauriwa na kila mtu, sio mtu wa kuyumbishwa,’’anaeleza.

Mpaji Abass Yussuf anafahamisha kuwa Mkunga mcheshi, nimpenda kujichanganya na watu hachagui, ingawa kwenye kutetea hoja huweka mbali utani.

                                      TAMWA

Kaimu Mratibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar, ofisi ya Pemba Amina Ahmed Mohamed, anasema wapo wanawake kadhaa, waliowapa elimu ya kugombea, akiwemo Mkunga.

Anasema wamekuwa na miradi kila baada ya muda, ukiwemo wa wanawake na uongozi SWIL, ambao uliwatoa wanawake wingi na sasa ni viongozi akiwemo Mkunga.

‘’Kwa mfano Waziri wa Habari, Mwakilishi wa Jimbo la Konde, huyo Mkunga, alikua mkuu wa Mkoa wa kaskazini Pemba ni kundi la wanawale waliopitia mikononi mwa TAMWA kwa baadhi ya wakati,’’anasema.

Anakikiri kuwa mafunzo hayo, sio tu kujifunza wao namna ya kugombea, lakini kujiamini, kujitetea, kutoa hoja na kufanyakazi kwa bidii.



Amina anasema TAMWA wakati mwingine huwa na miradi hata ya kuwawezesha waandishi wa habari, ili kuwaibua wanawake waliofanikiwa kama Mkunga na wingine, kwa lengo kuwaonesha jamii uwezo wao.

  KATIBA

Katiba ya Zanzibar ya mwaka1984 inatambua na kulinda usawa wa kijinsia katika uongozi kwa kuhakikisha wanawake, kama sehemu ya jamii, wanashiriki katika vyombo vya maamuzi.

Kwenye kifungu chake cha 21, kinasiistiza, ‘kila mzanzibari anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kupitia wawakilishi waliochanguliwa,

Hata kifungu cha 12, cha katiba hiyo kinabainisha kuwa, ‘haki ya usawa mbele ya sheria na wanayohaki bila ya ubaguzi wowote kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria’.

Mkunga Hamad Sadala (65) ni mtoto wa watano kwenye familia ya Hamad Sadala kwa sasa ndie makamo mwenyekiti ngome ya wanawake taifa kwenye chama cha ACT-Wazalendo na bado ana nia ya kujitupa jimboni mwaka 2030.

                  Mwisho

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...