NA TATU MAKAME, ZANZIBAR@@@@
WAZIRI wa fedha Tanzania Balozi Khamis Mussa Omar amesema Mamlaka hiyo inatarajia kukusanya shilingi trilioni 42 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 katika maeneo mbalimbali ya Tanzania ili kuimarisha ukuaji wa uchumi hapa nchini.
Alisema hayo Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ikiwa ni muendelezo wa tamasha la Kizimkazi fastival.
Alisema mapato hayo kutoka vyanzo vya ndani kwa robo tatu ikiwemo ulipaji kodi kwa wafanyabiashara na kueleza kuwa kwa mwezi ulioanzia Julai mwaka huu mamlaka hiyo ilikusanya zaidi ya bilioni 800 sawa na ongezeko la asilimia 21 ya makusanyo.
Alisema ukusanyaji mapato unaimarika kila mwaka kwani mwaka wa fedha 2024,2025 Mamlaka ilifikia asilimia 1003 huku mwaka 2025_2026 kiwango cha mapato kilifikia asilimia 1005 kwa Tanzania nzima katika maeneo yote ya yanayokusanywa kodi.
Aidha aliwataka wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiari kwani ukusanyaji huo wa kodi ni mzunguuko wa uchumi ambao utawezesha ujenzi wa miundombinu katika maeneo mbalimbali ya Tanzanzia.
"Tumejipanga kuimarisha mifumo na huduma kila mikoa kurahisisha ulipaji kodi kwa wafanyabiashara", alisema.
Alieleza kuwa katika kikao cha bajeti cha kuu ya serikali mwaka huu kilichofanyika Bungeni Dodoma serikali iliamua kutenga mfuko maalum ambao utakaotumika kwa ujenzi wa miundombinu kama ujenzi wa barabara,skuli,maji,afya na huduma nyengine za jamii ikiwemo majengo ya Ofisi za serikali na kueleza kuwa fedha zitakazokusanywa na TRA asilimia 70 zitumike kwa ujenzi wa shuhuli hizo za kijamii.
Sambamba na hayo alisema kati ya fedha zitakazokusanywa shilingi bilioni 5 60 zitatumika kwa ujenzi wa nyumba za watendaji wa mamlaka hiyo sehemu za mipakani lengo kurahisisha ukusanyaji wa mapato pamoja na kuongeza ufanisi kwa watendaji hao.
Alisema kazi inayofanywa na mamlaka hiyo ya kuwahimiza wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiari imelenga kuendelea ujenzi kwani ukuaji huo ni ishara ya kukua kwa uchumi wa Tanzania.
Alitumia nafasi hiyo kueleza kuwa ukuaji wa uchumi umechangia ujenzi wa miradi ya maendeleo katika sekta mbalimba hasa ujenzi wa skuli,barabara ,afya na huduma nyengine za jamii.
Nae Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA )Yusuph Juma Mwenda akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya TRA Kizimkazi alisema ujenzi huo wa ghorofa moja utatoa huduma kwa wakaazi wa Kizimkazi na Paje pamoja na maeneo mengine ili kusogeza huduma za ulipaji kodi kwa wafanyabiashara.
Alisema ofisi hiyo itagharimu shilingi bilioni 3,6,000,000 hadi kukamilika kwake na kueleza kuwa ofisi kama hizo zimejengwa katika mikoa zaidi ya 33 ya Tanzania na kueleza kuwa kila wilaya ujezni wa Ofisi hizo utaendelea.
Sambamba na hayo aliwapongeza wakandarasi wa ujenzi kwa jengo hilo linalokwenda kwa kasi na kueleza kuwa kumalizika kwake kutarahisisha utoaji huduma.
Nae mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Othman Ali Maulid akimuwakilisha mkuu wa mkoa wa mkoa wa kusini Unguja Hamida Mussa Khamis alisema mkoa huo uko salama katika kuimarisha ulinzi na usalama.
Aliwapongeza viongozi wakuu wa nchi kwa kuimarisha miundombinu ya sekta mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa barabara na sekta nyengine za kijamii.
MWISHO

Comments
Post a Comment