Skip to main content

DIWANI FATMA ''KITOTO'' WADI YA TIBIRINZI: NA SAFARI YA UONGOZI HILI ALITAHADHARISHA KWA WENZAKE

 


 NA MARYAM SALUM, PEMBA@@@@

MWA NASIASA hatakiwi kuwa mbaguzi, watu wote ni sawa, ili mwisho wa siku, jamii ikuelewe tu,’’anasema Fatma Khamis Juma Diwani wadi ya Tibirinzi.

 ‘’Tabia yangu hupenda kujichanganya iwe kwenye kijiwe cha kahawa, sokoni nipo, masikani za vijana nipo, na makundi mengine yenye rika tofauti.

Hii ni kauli ya Fatma Juma Khamis, anayehudumu udiwani wadi ya Tibirinzi, Jimbo la Chake chake, kwa kipindi cha pili mfululizo sasa.

Katika siasa, mtu hatakiwi kuwa mbaguzi na badala yake awe kuwa karibu na jamii iliyomzunguruka, kwa maslahi mapana.

Anakiri kuwa kuingia kwenye kinyang’anyiro cha siasa, watu wote hupitia changamoto, ikiwemo kuitwa majina mabaya hasa kwa wanawake.

Kwenye jamii iliyo kubwa, tafsiri iliyopo, pindi mwanamke akiingia kwenye siasa hubandikwa majina maovu na yenye kukatisha tamaa, au kuwindwa na washindani wake.

Diwani Fatma anasema, kwa awamu ya kwanza ya udiwani wake, hakuishia kuomba kura kwa mikutanao ya hadhara pekee, bali alifuata utamaduni wa nyumba kwa nyumba.

“Katika mbinu zangu za kusaka udiwani wa mwaka 2020, niliamua kwenda mlango kwa mlango, na sitosahau nilipokosea kuondolewa uhai wangu, baada ya kutaka kupigwa panga kwa nyakati za usiku, na muombezi wangu ilikuwa ni mbio,” anasimulia.

Kwa siku hiyo, msaka udiwani huyo, baada ya kuwahadithia wachache, walimshauri aende polisi kutoa taarifa na chamani kwake, ili kuachia ngazi nafasi hiyo, jambo ambalo alisita.

“Changamoto hiyo niliyokumbana nayo mwaka 2020, ilikuwa mbolea kwangu, na ilinitia ari ya kutafuta uongozi, na hadi sasa nahudumu udiwani wadi ya Tibirinzi, kwa awamu ya pili”, anaeleza.

Bado anashangaa, kuwa bado wapo baadhi ya watu, wanadhana kuwa, mwanamke hawezi kuwa kiongozi, wakinasibisha na uhuni, kuacha utamaduni na kuitupa familia, jambo ambalo sio sahihi.

“Mimi ni mama wa familia ya watoto wanne, na kushughulikia wazazi wengine, lakini bado sijateteresha familia yangu wala udiwani wangu, haujaingia kasoro.

ALIWAZAJE UONGOZI DIWANI HUYU

Fatma Khamis Juma ambaye ni mrefu wastani, mwekundu mwenye paji la ucheshi, alianza kuusaka uongozi, tokea ngazi za vijana.

Kwa wakati huo, akiwa ndani ya chama cha Mapinduzi hakuishia kuwa mwanachama wa kawaida, alianza kupanda daraja za kufika juu, kwa kugombea nafasi za chini.

“Wakati nilipokuwa mwanachama wa Uomoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi, sikuridhika kuwa mwanachama wa kawaida, na hapo niliusaka ukatibu na uwenyeketi wa vijana ngazi ya tawi, na kufanikiwa,” anasimulia.

Kumbe kila siku zikienda mbele, zikilikuwa zikimpa ujasiri, kujiamini, kumuonyesha njia na kumpa nguvu ya kutaka uongozi, hadi sasa akiwaongoza wananchi 3,000 wadi ya Tibirinzi.

Ujasiri wa diwani huyo, haunekani tu kwenye nafasi hiyo, bali hata kwenye mikutano ya kawaida ya kijamii, au ya kitaasisi, husimamia msimamo wake, wenye tija kwa taifa.

“Hata nilipokuwa masomoni, nilianza kuwa mtetezi wa wenzangu, ili wasionewe, na wakati mwingine hadi kufika kwa Mwalimu mkuu, ili kutaka ufafanuzi wa jambo,” anakumbuka.

HEKAHEKA ZA UDIWANI AWAMU YA PILI

Mwaka 2025, Diwani huyo machachari, alizikwea tena ngazi za CCM, wilaya Chake chake, kwenda kuchukua fomu, ili kuwaongoza tena wananchi wa wadi ya Tibirinzi.

Baada ya mchakato mzito wa ndani ya chama, hatimaye Fatma aliibuk tena na ushindi, na kukabidhiwa bendera, ili kuusaka udiwani kwenye uchaguzi mkuu.

Hapo ikawa ni mikutano ya hadhara ya kampeni, kutembea kwa miguu, gari za matangazo na kurejea tena, kuwafikia wananchi uso kwa uso, ili kuwaomba kura.



Wakati wa matokeo ya uchaguzi, wanachi kwa mara nyingine walimuamini, na ndio maana wakaamua kumchagua tena, kushika hatamu ya udiwani Tibirinzi.

CHANGAMOTO ALIZOKUSUDIA KUZIPATIA UFUMBUZI

Diwani Fatma anasema, wakati wa kampeni aligundua ukosefu wa huduma ya maji safi na salama, kwa baadhi ya vijiji, utoro wa wananfunzi, matumizi ya dawa za kulevya, na mitaji midogo kwa wajasiriamali.

“Viongozi wote wanajali sana shida za wananchi, lakini akiwa kiongozi mwanamke kama mimi, huwa tunajali mara dufu, shida zao,” anasimulia.

YALIYOJIRI BAADA YA KUWA DIWANI

Sasa Diwani Fatma Khamis Juma, anakiri kuwa huduma ya maji safi na salama, kwa kushirikiana na serikali kuu, katika baadhi ya vijiji, imeshakuwa historia.

Kuhusu matumizi ya dawa za kulevya kwenye wadi hiyo, hivi karibuni amesharikiana na mamlaka husika, kutoa elimu katika vijiwe sugu, na baadhi yao kushikiliwa na vyombo vya kisheria.

“Nilikusudia nikiwa Diwani utoro wa wananfunzi iwe skuli au madrassa, nao umebaki historia, na sasa baadhi ya maeneo yanaridhisha ikiwemo Wesha, na Ndagoni”, anasema.

  WANAOFANYA KAZI NA DIWANI FATMA

 Mstahiki Meya, Manispaa ya Chake Chake, Suleiman Makame Ali, anasema kuwa wadi ya Tibirinzi ilimpima Fatma kutoka uongozi wake wa awamu ya kwanza, na kumuona anafaa, ndio maana awamu ya pili, akarejeshwa tena.

“Zipo wadi kadhaa wilaya ya Chake Chake, zimeshapiga hatua ya kimaendeleo, kwa huduma mbalimbali kuimarika, ingawa hii ya Tibirinzi mwenyewe kaja”, anasema.

Meya huyo anaeleza kuwa, Wadi ya Tibirinzi ni kubwa, ingawa ukubwa huo na aina ya Diwani aliyepo, utendaji wake wa kazi ni zaidi ya utendaji wa baadhi ya wanaume.

Sheha wa Msingini Mkubwa Ali Kombo anakiri kuwa, wadi yao kwa wamu ya pili mfululizo, imepata kiongozi mwenye maono, ujasiri na kutimiza ahadi zake kwao.

“Mfano, shehia yetu zipo huduma za ujenzi wa njia za ndani, ikiwemo ya Msingini kupanda juu, katika kijiji cha Mitambuuni, na huduma ya maji safi na salama, ambazo zimeshajengwa utawala wa diwani huyu,’’anasema.

Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Chake Chake Mayasa Amani Vuai anakiri kuwa, katika wadi 10, zote zimetimiza malengo, ingawa ya Tibirinzi, iko juu zaidi.

“Wadi ya Tibirinzi inang’ara kwa huduma za kijamii na hapa, nathibitisha kweli mwanamke akipewa madaraka, wananchi huneemeka,’’ anasimulia.

                  WANANCHI WA TIBIRINZI WANASEMAJE

Nunuu Mwalim Ngwali anasema Diwani huyo, amekuwa akimfahamu, tokea ujana wake kwa uchakarikaji na kusimamia misimamo yenye tija.

“Kwa awamu ya kwanza, alipotangazwa kuwa Diwani, sote tulifurahika maana ukakamavu wake, mbio zake, ujasiri na kuchangamka na kila mtu, tulijua kuna shida zitatuondokea”, anasema.

Ali Kombo Khamkis anakiri kuwa, ujio wa Diwani Fatma, wadi ya Tibirinzi imepata heshima kubwa ya kimaendeleo, ni tofauti na awamu zilizopita.

Anakiri kuwa, wameshapita madiwani kadhaa tena wanaume, na walihudumu kwa vipindi tofauti, walizikuta shida na waliondoka na kuziwacha ndani ya wadi.

Maryam Mohamed Said, anaona kuwa wakati umefika, kwa mfano wao ndani ya wadi ya Tibirinzi, nafasi za ngazi ya maamuzi viongozi wanawake, wakapewa fursa zaidi, kwani wanajicho la huruma.

“Naamini kuwa wadi nyingi za wilaya ya Chake Chake, zimefanya vizuri kwa kuwepo miradi mikubwa na ya kimaendeleo, ingawa wadi yao, inaongoza hasa baada ya kupata Diwani mwanamke”, anasimulia.

                       WANAHARAKATI

Mkurugenzi Mtendaji Jumuiya ya Tumaini jipya Pemba (TUJIPE) Tatu Abdalla Msellem, anasema kwa sasa wanawake, wamekuwa wakiaminiwa na wapiga kura, kutokana na matokeo mazuri ya baadhi ya wachache, walioshika hatamu.

Anasema wanaendelea kuielimisha jamii, hususani wanaume, kuhusiana na umuhimu wa kuwaamini viongozi wanawake, kuanzia ngazki ya familia hadi taifa, kwa mifano iliyo hai.

“Hata hapa Pemba, yapo majimbo, shehia, na wadi zinang’ara kwa miradi ya maendeleo, na ukiyafuatailia walioshika hatamu ni wanawake”, anasema.



Kaimu Mratibu Chama cha Waandishi wa Habari Wananwake Tanzania TAMWA -Zanzibar, Ofisi ya Pemba, Amina Ahmed Mohamed, anakiri kuwa nguvu zinazoendelea kuchukuliwa na TAMWA, wanaharakati, serikali kuu na wadau wake, juu ya kuwapa nafasi wanawake, zimefanikiwa kiasi.

 Anasema kwa miaka ya hivi karibuni, walau wanawake wanaonekana katika baadhi ya nafasi ya uamuzi, kuanzia udiwani, usheha, uwakilishi na ubunge, jambo linalotia tamaa kuelekea sera ya 50 kwa 50.

“TAMWA imekuwa na miradi kadhaa, ya kuwawezesha wanawake kutambua haki na wajibu wao, na kuieleza jamii nafasi ya mwanamke katika kuongoza, iwe ngazi ya familia, kijiji, mtaa wilaya mkoa hadi taifa”, anaeleza.

                              VIONGOZI WA DINI

Sheikh Said Abdalla Nassor wa Ofisi ya Mufti Pemba, anasema katika uislamu, wanawake wanaweza kuwa viongozi katika nyanja nyingi za elimu, jamii, na maendeleo.

“Wanawake wengi wamekuwa wanazuoni, walimu wa dini na wahifadhi wa hadithi katika historia ya uislam, hivyo kuwepo diwani mwanamke inaongeza uwajibikijai,’’anasema.

Katika eneo jengine,  Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kifungu cha 21(1), kinabainisha kuwa ‘kila Mzanzibari anayohaki ya kushiriki, shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja, au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa kwa hiari’.

Mkoa wa kusini Pemba, unaoundwa na wilaya za Chake chake na Mkoani, unayo majimbo tisa na wadi 16, ambapo kati ya hizo wadi tatu pekee, zinazoongozwa na wanawake, ikiwemo Tibirinzi.

                                     MWISHO.

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...